Zinazobamba

WANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI WAANZA MITAHANI YAO LEO,PIA SERIKALI YAFAFANUA UKWELI WA KUFUTWA KWA DIPLOMA YA UALIMU,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
Jumla ya wanafunzi 435,221wa kidato cha pili nchi nzima leo  wametarajia kuanza mitihani yao ya taifa ya kidato cha pili.
Ambapo kati yao wavulana ni 214,013 sawa na asilimia 49.17 na wasichana 221,208 sawa na asilimia 50.83.
Mbali na hao wapo wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao watahiniwa wasioona ni 67 na watahiniwa wenye uoni hafifu ni 306 ambao watapewa maandishi ya karatasi hukuzwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa Baraza la Mitihani nchini,Dkt Charles Msonde amesema mtihani huo ambao umeanza mapema hii leo ambao unatarajia kumalizika Nombemba 25 ya mwaka huu.


Amesema mtihani huo unalengo la kuwapima uwezo na uelewa kwa wanafunzi katika yote wajifunzayo kwa miaka miwili ya masomo yao huku wanafunzi wanaofeli wanakosa nafasi ya kuendelea na kidato cha tatu.
Dkt Msonde amesema maandalizi yote ya mtihani huo yamekamilika ikiwemo kusambazwa kwa mitihani itakayotumika katika upimaji huo pamoja na nyaraka muhimu katika mikoa na halmashauri zote ndani ya Tanzania bara.
Hata hivyo,Dkt msonde amesema Jumla ya wanafunzi 10,045,99 wanatarajia kuanza mitihani ya darasa la nne mwaka huu siku ya tarehe 23 na 24 Novemba ambapo kati yao wavulana ni 507,732 sawa na asilimia 48.54 na wasichana na 538,267 sawa na asilimia 51.46.
Pamoja na hayo dkt msonde amewataka wanafunzi pamoja na wasimizi kutohusika na vitendo vya udanganyifu huku akisema hatua kali za kisheria kwa waliohusika
 Pamoja na hayo Dk Msonde amefafanua kuwa mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi ngazi ya stashahada yamefutwa lakini wanafunzi waliopo vyuoni watamalizia masomo yao kwa muda uliobaki.

Dk Msonde amesema mafunzo hayo ya walimu yataendelea kwa utaratibu wa zamani ambao ulikuwa ngazi ya cheti.

Amesema usimamizi wa mitihani hiyo itakuwa chini ya Necta kama ilivyokuwa zamani badala ya Nacte.

"Wanafunzi walio vyuoni wataendelea na mafunzo hayo, isipokuwa kuanzia mwaka huu hatutadahili kwa ngazi ya diploma, tutadahili ngazi ya cheti kama ilivyokuwa zamani," amesema Dk Msonde.