WAIDAIWA SUGU WA BODI YA MIKOPO WAPEWA SIKU 90,SOMA HAPO KUJUA
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema kuwa
hadi sasa kuna jumla ya wadaiwa sugu 142,470 wenye mikopo ya shilingi
239,353,750,170.27 iliyokwishaiva hawajajitokeza wala kuanza kulipa mikopo yao.
Akitolea ufafanuzi wa maana ya neo "Wadaiwa
Sugu", Badru amesema kuwa ni wanufaika waliokopeshwa, muda wa matarajio
ukapita bila kuwasilisha taarifa zao na kulipa madeni ya mikopo waliyokopeshwa
tangu mwaka wa masomo 1994/1995.
Kuhusu hatua zinazochukuliwa na bodi hiyo, Badru
amesema mbali na kutoa siku 30, bodi hiyo inakamilisha taratibu za kuwafikisha
mahakamani kwa kuvunja sheria ya bodi ya mikopo kifungu cha 19A(1).
Hatua nyingine ni pamoja na kuyawasilisha majina
hayo katika taasisi za mikopo, kuwasiliana na wadhamini wao pamoja na
kuyatangaza hadharani majina ya wadaiwa sugu wote ili waajiri, wadhamini na
wadau wengine wayajue na kutoa taarifa katika bodi hiyo.
Kuhusu takwimu za mikopo iliyotolewa, amesema tangu
1994/95 hadi 2015/16 jumla ya shilingi 2,595,932,575.56 zimekopeshwa kwa jumla
ya wanufaika 379,179.
Amesema kati ya mikopo yote iliyokopeshwa, mikopo
iliyoiva ni shilingi 1,425,708,285,046.48 kwa wanufaika 238,430 ambao tayari
wamemaliza kipindi chao cha matazamio.
Badru amesema kuwa jumla ya wanufaika wa mikopo
93,500 wamebainika na kupelekewa ankara za madeni yao, ambapo kati yao
wanufaika 81,055 wanaendelea kulipa.