VITA RC MAKONDA NA KAMANDA SIRRO YAFIKIA PATAMU,JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU YAINGILIA KATIK,SOMA HAPO KUJUA
Jeshi la polisi nchini limesema litafanya uchunguzi
wa tuhuma za rushwa dhidi ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamanda Simon Sirro na baadhi ya makamanda wa mikoa akiwemo kamanda wa mkoa wa
Kinondoni Susan Kaganda.
Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Robert Boaz katika makao makuu ya Polisi
jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo ya CP Boaz kwa niaba ya jeshi la polisi
imetolewa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hivi karibuni
kuwatuhumu makamanda hao kuwa wanasita kuwachukulia hatua watumiaji na wauzaji
wa kilevi cha shisha kwa madai kuwa huenda wakawa wamepokea rushwa kutoka kwa
wanaojishughulisha na biashara hiyo.
Makonda alitoa tuhuma hizo licha ya yeye ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama katika kanda hiyo kutoa maagizo wahusika
kuchukuliwa hatua.
CP Boaz alisema, kuhusu tuhuma ya rushwa suala hilo
lina taasisi zake zinazohusika, na kwamba jeshi hilo limepokea tuhuma hizo
dhidi ya askari wao kwa hiyo watazichunguza kubaini ukweli.