SKATA LA RC MAKONDA KUMTUHUMU KAMANDA SIRRO KULA RUSHWA ZA WAFANYABIASHARA WA SHISHA ,SIRRO AIBUKA NA KUSEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es salaam Simon Sirro,
amesema kama Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ana wasiwasi na Jeshi
la Polisi katika operesheni ya kutokomeza matumizi ya Shisha, achukue hatua
zaidi kwa sababu yeye ni kiongozi wao na ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
Usalama Mkoani Dar es salaam.
Akiongea kupitia kipindi cha Sun Rise cha Times Fm
leo asubuhi, Sirro amedai wao kama jeshi la Polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa
Sheria na Operesheni ya kutokomeza Shisha jijini inaendelea kama kawaida
kilicho baki ni Mwanasheria mkuu wa Serikali kuandaa mashtaka kwa Watuhumiwa.
“Watu wamekamatwa ni wengi, kimsingi
kazi inafanyika, sasa huo ni wasi wasi kama wasi wasi basi unabaki kuwa wasi
wasi, kikubwa niseme tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni, yeye ni
mwenyekiti wangu wa kamati ya ulinzi na usalama kwa hiyo ninaamini kama ana
wasiwasi na chombo chake najua atakuja kutuita na kutuambia nini cha kufanya.
“Lakini kama ana wasi wasi Zaidi yeye ni
kiongozi wetu atajua atachukua hatua gani dhidi ya sisi, kwa hiyo namuachia
mkuu wangu wa kazi yeye ndio atajua nini cha kufanya”
Akitolea ufafanuzi kama alipatiwa taarifa juu ya watu
10 waliotaka kumpa ‘Mlungula’ Mkuu wa Mkoa ili kumziba ‘Mdomo’ kukemea matumizi
ya kilevi cha Shisha, Kamanda Siro alisema hawezi kulisemea lolote swala hilo
na amemtaka Mtangazaji wa Sun Rise Stanslaus Lambat amuulize Mh Makonda taarifa
aliipeleka wapi na si yeye.
Post Comment