RAIS MAGUFULI AENDELEA KUTEUA TU WATENDAJI,AMPA ULAJI JAJI WARIOBA,SOMA HAPO KUJUA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli leo tarehe 18 Novemba, 2016 amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Bw. Diwani Athuman kuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Kagera.Uteuzi wa Bw. Diwani Athuman unaanza mara moja.
Wakati huo huo,
Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika taasisi tano za
Serikali kama ifuatavyo.
Kwanza, Rais
Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji
Joseph Sinde Warioba kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.
Pili, Rais Magufuli
amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) na amemteua Bw. Sylvester M. Mabumba kuwa Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016
Tatu, Rais Magufuli
amemteua Prof. Patrick Makungu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO).
Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.
Nne, Rais Magufuli
amemteua Bw. Martin Madekwe kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.
Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.
Tano, Rais Magufuli
amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la
Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki Tanzania (TPRI)
Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
18 Novemba, 2016