SAKATA LA SERIKALI KUMGOMEA MCHUNGAJI RWAKATALE KUWATOA WAFUNGWA MAGEREZANI,MREMA AMWANGUKIA MAJALIWA,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole,Dkt. Augustine
Mrema amemwandikia barua Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mh. Kasim Majaliwa kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango wake wa
kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha na wasamalia wema baada ya
kukidhi vigezo.
Dkt. Mrema ameyasema hayo mchana huu wakati wa kutoa
taarifa yake hiyo kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuzungumzia
suala lake hilo la Maafisa wa Magereza kusitisha hatua ya kukatisha mpango wake
licha ya kuwalipia wafungwa waliokidhi vigezo.
“Mimi nimeona nisinyamaze. Napaza sauti nataka Rais
aone, ajue kama magereza yetu yanashida na tunalotatizo kwa nini mpango huu
umesimamishwa na umesitishwa tumekosea wapi?.
"Nimesha muandikia barua Waziri Mkuu
kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43 tayari tumesha
walipia faini hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota. Mrema amefanya kosa
lipi? Ama Mama Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka wamesitisha
zoezi hili” amesema Mrema kwa waandishi wa habari.
Dkt. Mrema ameweza kuonyesha nyaraka ikiwemo risiti
mbalimbali walizofanya malipo kwa ajili ya kuwatoa wafungwa hao ambapo amesema
haki ya kuzuia mpango huo imeweza kumuumiza vibaya kwani wasamalia wema
walioweza kujitolea fedha za mpango huo imewagusa pia.
Pia ameongeza kuwa, mpaka sasa magereza
mbalimbali kuna msongamano wa wafungwa ambao wanahitaji msaada wa kutoka ila
hawajapata fedha za kulipiwa hivyo pindi wasamalia wema kama Mchungaji Mama
Rwakatare wanapojitokeza wanatakiwa kupongeza na wala si kupinda kona kona.Hivi
karibuni Jeshi la Magereza lilisitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa na
Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko magerezani hadi
hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.
Awali ilidaiwa kuwa Mpango huo unaofanywa na
Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine
Mrema tayari umewezesha wafungwa 78 kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini
inayofikia Sh25 milioni.
Kwa mujibu taarifa zilizonukuliwa katika moja ya
vyombo vya habari hapa nchini vilieleza kuwa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma,
Antonio Kilumbi alisema amepata maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka
ngazi ya juu ya jeshi hilo na kuongeza kuwa, wananchi wengine bado
wanaweza kuwalipia faini hiyo ndugu zao.
Hata hivyo Mrema alisema mpango huo ulilenga
kupunguza msongamano magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia
wafungwa hivyo kusitisha unarudisha nyuma juhudi za Bodi hiyo ya Parole katika
kuwasaidia wafungwa waliokizi vigezo