Zinazobamba

BENKI YA NMB YAIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI NCHINI,SOMA HAPO KUJUA





https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUMPigMSqD4WTGXCjUur4mB7DwO4ErZFrdpT06Kz9Vqcy0gSTLNC0WKKskhjjXtzw-Sf7nOqlXq-KuuPYIzY3AZ1Omn55SxDWpHfH9MUGI-vuJ2iknPx5zbSwALzjb9GUqRWo8LwC2nO9m/s1600/1%25281%2529.JPG Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi, George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea madawati kutoka NMB leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixBB409HgIodghASbw5E-qXRZCs_9BCxJH_umjaiLvYFBqagZYSM-AF6WgkRHszYxJ1lryDDGYsn0eskLF8UhjlHVLidTEapS7RbhVcKpxgD-2Caof3vwo_4-Jdx6ZbsT_vwx9IyEsPypp/s1600/2%25281%2529.JPG
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi madawati kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.



BENKI ya NMB imetoa msaada wa madawati 3500 kwa serikali yenye thamani ya sh. Bilioni 1.5 ya madawati yote ambayo walikuwa wameahidi kutoa tangu 2014 ikiwa ni jitihada ya kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafunzi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa madawati, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais -Tamisemi, George Simbachawene amesema benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kusaidia katika elimu.

Simbachawene amesema kuwa madawati hayo yatapelekwa katika mikoa ambayo haijaweza kumaliza tatizo la madawati ya kwa baadhi ya shule.
Amesema kuwa kuna baadhi ya mikoa imemaliza tatizo la madawati hivyo kutokana na msaada huo utasaidia sehemu kubwa kumaliza tatizo la madawati.

Madawati hayo yatakwenda katika shule za msingi na sekondari 71 kwa kila shule kupata madawati 50.
“Nashukuru kwa msaada huu katika mapambano ya upungufu wa madawati nchini,  baada ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuagiza ya kuwa hakuna mwanafunzi kukaa  chini tumefanikiwa na kubakiza wilaya chache ambapo madawati haya yatakwenda” amesema Simbachawene.