SAKATA LA DANGOTE KUFUNGA KIWANDA CHAKE,SHIRIKA LA TPDC LAIBUKA NA KUSEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
HUKU kukiwa kuna taarifa kiwanda cha uzarishaji na
uuzaji saruji cha (Dangote)kilichopo mkoani Mtwara kitangaza kusitisha uzarishaji wa saruji hiyo kwa kile
inachoelezwa kuwa shirika la Maendeleo
ya Petroli nchini (TPDC)limeshindwa kuwauzia gesi asilia kwa bei rahisi
kwenye kiwanda hicho.
Nalo,Shirika la TPDC limeibuka na kukunanusha taarifa hiyo
na kusema shirika hilo limefanya jitihada mbali mbali za kuhakisha kiwanda cha
Dangote kinapata nishati ya gesi.
Pia shirika hilo limesema limekuwa likifanya vikao
mbali mbali na kufanya makubaliano yaliofanyika baina yao na mwekezaji huyo ili
kuhakikisha wanaridhia nia yao ya
kutumia gesi asilia ya kuzalisha umeme kwa ajili ya kiwanda cha sajuri ambacho
kipo Mkoani Mtwara ambacho kinatajwa kuajiri watanzania wengi.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam,Kaimu wa nisharti na Madini,John Shija
amesema TPDC hufuata kanuni na utaratibu wa kupanga bei ya gesi asilia
ambapo hupanga kulingana na aina ya mteja ,huku akidai wateja wamegawanyika
kufuatia makundi tofauti kama vile wateja wa viwandani,majumbani,magari pamoja
na wateja wa kuzalisha umeme.
Ameeleza kuwa hata hoja bei ya gesi asilia,huwa inapendekezwa na TPDC lazima iridhiwe na ipitishwe na EWURA ndipo
ianze kutumika.
“Dangote kama mtumiaji wa matumizi ya viwandani amekuwa na mazungumzo na sisi kwa
mdamrefu kuhusu bei ya gesi asilia,na hiko kiwanda kimeomba kupewa gesi asilia
kwa bei ambayo hapa kwetu Tanzania ni kidogo kwani kiasi hicho cha bei ndicho
kinacholipwa kununuliwa gesi ghafi kutoka kiwandani”amesema Shija.
Hata Hivyo,Shija amesema shirika hilo limeshafanya mikataba ya awali na kiwanda hicho kwa ajili ya kuwauzia gesi asilia
itakayotumika kuzalishia umeme utakuwa unatumika katika kiwanda cha Dangote.
Huku akidai kuwa mpaka mwezi January 2017
miundombinu ya gesi asilia itakuwa imeunganisha na mitambo ya kufua umeme
utakaotumiwa na kiwanda hicho.
Shija amesema shirika la mafuta ya Taifa limekuwa
linafanya kazi zake kwa kufauata sheria ,kanuni na taratibu za nchi,pamoja na
kuwajali wawekezaji akiwemo Dangote ili
wawekezi katika kukuza uchumi wa nchi.
Pamoja na hayo,Shija ameitaka jamii kuacha kuzusha
taarifa ambazo hazina mantiki.