RAIS MSTAAFU KIKWETE KUWATUNUKU SHAHADA MBALI MBALI WAHITIMU WA UDSM KESHO,YUMO PIA MZEE MBEKI,SOMA HAPO KUJUA
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete kesho anatarajiwa kumtunuku shahada ya Heshima ya Udaktari ya chuo
kikuu cha Dar es salaam (UDSM)mpigania uhuru na mwanaharakati mashuhuri ambaye
ni Rais mstaafu wa Jamhuri ya Afrika Kusini Thabo Mbeki.Anaandika KAROLI
VINSENT endelea nayo.
Mbali na Kiongozi huyo,Pia Kikwete anatarajiwa kuwatunuku
shahada mbali mbali watahitimu 6717 ambao wamemaliza masomo yao katika chuo
hicho,
Ambapo kati yao kati yao 61 wanatunukiwa Shahada ya
Uzamivu, 627 Shahada za umahiri na 59 Shahada ya Uzamili huku wahitimu 5968
Shahada za awali.
Profesa Rwekeza Mukandala ambaye ni Makamu mkuu wa chuo
UDSM amewaamia waandishi wa habari kuwa amesema kuwa Mahafali hayo yataenda
sambamba na kusimikwa rasmi kwa Dk. Jakaya Kikwete kuwa Mkuu mpya wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Profesa
Mkuandala amesema Mbeki amekubali kupokea tuzo hiyo ya heshima na atahudhuria
awamu ya kwanza ya mahafali ya 46 ya Chuo kikuu cha Dar na anatunukiwa tuzo
hiyo kutokana na mchango mkubwa na wakipekee katika kupigania haki bara la
afrika