Zinazobamba

RAIS MAGUFULI AWAPUUZA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NA WANASIASA,AENDELEA "KUMKUMBATIA" RC MAKONDA,SOMA HAPO KUJUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdcydp_kz_nmohVMerjPHfTXgOCxfWoZ9TwgY8m8Q_mg7uMcTWNcvrtVzABmewvqDvXb8xWXAEu1aA8HizCNX-ml4MDEgfkFCxpxLOEwHjGiwbquWk2XXUOKkjIiWq7zWIiteGCsofBseN/s1600/WhatsApp+Image+2016-11-25+at+11.25.01.jpeg

NA KAROLI VINSENT
WAKATI wanasiasa,wananchi na watetezi wa Haki za Binadamu wakiwa wanazipinga hatua za mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda   kwa watumishi wa umma,kwa kile wanachosema kiongozi huyo anakikuka misingi ya haki za biandamu kwa hatua yake ya kutoa kibali cha kukamatwa kwa watumishi na watendaji wa serikali bila ya hata uchunguzi juu ya tuhuma zinazobuliwa kwa watendaji hao,

Naye Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo ni kama naye ameonesha kuwapuuza watu hao,baada ya kumpigia simu Makonda na kumpongeza kwa  anayoyafanya na kumruhusu aendelea na kazi ya yake ya kufukuza watumishi wa umma.

Rais Magufuli ambaye alimpigia mkuu huyo wa mkoa wakati alipokuwa akisikiliza kero za Wananchi katika Kata ya Mbezi Luis eneo la Malamba Mawili ambako aliweza kumsisitiza kuwa aendelee kutumbua watu huko huko aliko.


“Endelea hivyo kutembelea wananchi na kutoa ufafanuzi kwa sababu nyingine ufafanuzi huu kama ungetolewa mapema wala wananchi wasingekuwa na sababu ya kuja kuuliza maswali kui kwa hiyo endeleeni hivyo hivyo na juhudi za Dar es Salaam na wakuu wa Wilaya yako na watendaji wote kwa kazi nzuri mnazozifanya kwa kusikiliza kero zao bila kujali vyama vyao bila kujali makabila yao na uendelee kutumbua huko huko” Amesema Rais Magufuli.

Amemtaka pia kuendelea kupiga kazi na kumwabia kuwa yeye yupo nyuma yake kwani amevunja mwiko wa viongozi waliokuwa wanapendelea kukaa ndani.

Kwa upande wake mkuu huyo wa mkoa aliendelea kuwa mtiifu huku akimsikiliza Rais Magufuli kwa Makini juu ya pongezi anazopewa mbele ya watu kwani ameweza kurudisha imani kwa viongozi wa serikali ambayo iliondoka kwa watu kutokana na ujinga wa watu wa chache. Mhe. Makonda.