SHIRIKA LA NDUGE LA ATCL LAENDELEA KUFAGIA WAFANYAKAZI,YAWAONDOA WAKURUGENZI WAKE,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL,Mhandisi Emmanuel Korosso(katikati) akizungumza na
Waandishi wa Habari leo katika Ofisi za Shirika hilo,Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika,Ladislaus Matindi,kulia ni Mjumbe wa Bodi,Dkt. Mussa Mgwata
|
BODI ya shirika la ndege nchini(ATCL) imeagiza
kuondolewa baadhi ya mameneja katika nafasi zao ndani ya shirika
hilo baada ya kubainika wanautendaji
dhaifu pamoja na kuwepo na viwango
vidogo vya elimu visivyokidhi katika nafasi hizo.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hata hivyo,Bodi hiyo imetangaza kuzindoa idara tano za ukurugenzi ndani ya shirika
hilo baada kubainika pia hazina tija,
Idara hizo ni kurugenzi ya idara ya Biashara,Kurugenzi ya dara ya
Ufundi,kurugenzi ya idara ya oparesheni,kurugenzi ya idara usalama pamoja na
kurugenzi ya idara ya fedha.
Huku pia Bodi hiyo ikitoa maelekezo kwa wakurugenzi
wote waliokuwa wamekaimu katika idara hizo ambazo zimeondolewa wametakiwa kurudishwa katika nafasi za
chini ambazo sio Menejimenti
Akitangaza maazimio hayo ,leo Jijini Dar es
Salaam,Mwenyeti wa Bodi ya (ATCL),Mhandisi Emmanuel Korosso amesema mara baada
ya shirika hilo kupokea ndege mpya aina ya Bomardier Q400,na kuanza safari zake
sehemu mbali ndani ya nchi na nje ndipo wakaitisha kikao cha Bodi ya
wakurugenzi ya shirika hilo kwa lengo la kufanya uamuzi wa kimuundo wa
kuboresha shirika hilo.
Amesema Wameibaini kuwepo kwa wakurugenzi ndani ya
shirika hilo ambao ni wadhaifu pamoja kutokizi kielimu.
“Katika kiko chetu cha Novemba 18,tumebaini
watendaji hawa wanauwezo mdogo wa elimu
ambao mtu hawezi kuwa na elimu ndogo kiasi kile hakawa mkurugenzi,tena mbali na
elimu ni wadhaifu mnao kiutendaji kabisa na hatuwezi tukawa nao kwenye shirika
hili”,amesema, Mhandisi Korosso.
Mhandisi Korosso amesema Bodi yake imuagiza Mtendaji
mkuu wa (ATCL) Mhandisi Ladislaus
Matindi kuwaondoa wakuregenzi wanaokaimu nafasi zao na kupangiwa katika nafasi
za chini ambazo sio menejimenti au
kupangiwa katika vituo vya Mikoani.
Aidha,Bodi hiyo
katika kikao chake hicho ,ilipitisha mpango wa biashara wa muda (Interim
Business Plan) na Muundo wa muda (Interim organization Structure)ili kukizi
matakwa ya sasa ya ATCL kutokana na malengo iliyojiwekea katika kipindi cha
miaka mine.
Mbali na hayo Bodi hiyo imemuagiza Mtendaji wa
shirika hilo kutangaza nafasi zozote ambazo anaona kuwa kuna umuhimu wa kuajiri
watu wengine ili kuongeza kasi za ufanyaji kazi katika shirika hilo.
Mhandisi Korroso ameuagiza pia Mtendaji huyo
kutengaza mara moja