Zinazobamba

PROFESA MUKANDALA AAGA RASMI UDSM,SOMA HAPO KUJUA



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandala, ameiaga rasmi jumuia ya Chuo hicho baada ya kukitumikia kwa miaka 10, tangu 2006 alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

Sehemu ya hotuba yake kwenye mahafali ya 46 ya chuo hicho leo, Dar ilisema, "Nimekitumikia chuo hiki kwa miaka 10, leo hii ni mahafali yangu ya mwisho kuhudhuria kama Vice Chancellor wa UDSM, muda mfupi umebaki nipumzike nimpe kijiti mwenzangu, naamini atakuja mtu ambaye ataipeleka mbali zaidi UDSM."