Zinazobamba

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AJITOSA KUWASAIDIA VIJANA WALIOKOSA AJIRA,SOMA HAPO KUJUA

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/3349456/medRes/1411872/-/10laqxbz/-/PICHA+HAPI.jpg
Vijana wametakiwa kuondokana na mawazo ya kuajiriwa pindi wanapohitimu chuo kikuu bali wametakiwa kubuni nafasi ya kujiajiri au kubuni biashara mbali mbali jambo litakalowasaidia kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Hayo yamebainishwa leo na mkuu wa wilaya ya kinondoni,
Ally Hapi wakati wa ufunguzi wa  mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana zaidi ya 1000 ndani ya Halmashauri hiyo kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu na wasiowahitimu vyuo vikuu, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kubuni biashara na miradi mbalimbali.
Ambapo Hapi amesema serikali haina uwezo wa kuajiri wote wanaomaliza vyuo vikuu kutokana na ufinyu wa ajira uliopo jambo analowataka wahitimi hao kubuni mipango ya kujiajiri.

Amesema kuwa jukumu la serikali ni kuwakea mazingira mazuri kwa wahitimu hao ili waweze kujiari ndilo jukumu analolifanya yeye katika kutoa mafunzo kwa vijana ambapo ameleeleza kuwa ameanzisha mafunzo hayo kwa nia ya kuwaondoa uwoga vijana katika kujiajiri
Kwa upande wake vijana waliopata mafunzo hayo wamemshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kumuhaidi kutekeleza mafunzo hayo kwa vitendo