Naibu waziri mambo ya ndani awapa "siri" abiria wa ubungo, ataka madereva kuacha tabia ya kuvunja sheria za barabarani
Kuelekea msimu wa Krismasi na Mwaka Mpya Naibu waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi, Hamad Masauni amewataka abilia kuacha tabia ya woga na kuamua kuwafichua madereva wanavunja sheria za barabarani, akisisitiza kuwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza ajali zinazotokana na uzembe.
Akizungumza
katika kampeni maalum ya paza sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama
Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ubungo jijini Dar es Salaam.
Amesema
dereva kutojua sheria za usalama barabarani isiwe kigezo cha kuvunja sheria
zilizowekwa kutokana na waathirika wa ajali ni watanzania ambayo ndio nguvu
kazi ya taifa.
Amesema
kumekuwa na tabia ya madereva kutaka kuendesha mwendo kasi katika vipindi hivyo,
hivyo maabiria wanapaswa kufahamu kuwa huko ni kuvunja sheria na wanapaswa
kuwafichua.
Nae
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani , Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi
(DCP), Mohamed Mpinga amesema kampeni iliyozinduliwa ni jitihada za kikosi cha
usalama barabarani katika kupambana na ajali pamoja na kuongeza askari kila
sehemu ambayo dereva wamekuwa wakiuka sheria za usalama barabarani.
Amesema
abiria wanatakiwa kuwa chachu ya kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za usalama
barabarani kwa madereva ili waweze kuchukulia hatua.
Mjumbe
Usalama barabarani Mkoa Dar es Salaam, Idd Azzan amesema kampeni hiyo ni
italeta mageuzi katika kupunguza ajali.
PIX
1. 1.Naibu Waziri a izara ya Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni akizungumza jambo
katika hafla uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa
Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ya Mikoani na Nchi Jirani
cha ubungo jijini Dar es Salaam.
PIX.2
Mkurugenzi wa Sumatra,Gilian Ngewe akizungumza katika kampeni ya Paza Sauti
iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania leo jijini Dar es
Salaam.
Pix3.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi, Hamad Masauni akiwa Kamanda Kikosi cha Usalama Babarani (DCP),
Mohamed Mpinga ndani ya moja ya mabasi katika kituo cha Mabasi ya Mikoani na
Nchi Jirani cha Ubungo katika uzinduzi
wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA
Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Pix
4. .Masauni baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya usalama
barabarani inayoratibiwa na Mabalozi wa Uslama Barabarani RSA Tanzania leo
jijini Dar es Dar es Salaam.
Pix
5.Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azani (kushoto) ambaye pia ni mjumbe wa
kamati ya Usalama barabarani akifatilia hotuba ya mgeni rasmi hayupo pichani katika uzinduzi wa kampeni ya
Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania leo
jijini Dar es Salaam.
Pix
6.Baadhi ya wananchi waliohudhuria katiika katika uzinduzi wa kampeni ya Paza
Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania leo jijini Dar
es Salaam.
Pix
8 . Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandis Hamadi Masauni (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahamasihaji wa mauala ya ualama
barabarani na viongozi engine wa kamati za usalama barabarani.