Serikali yawashauri Benbros motors ,Yutong Zhengzhou kufungua kiwanda cha magari Tanzania
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Bw. Moses Nnauye akifurahia jambo mbele ya Wateja wa Kampuni ya Benbros. Aliyechuchumaa ni Injinia ufundi wa Kampuni hiyo Bw. Frank Lee |
Kampuni za Benbros Motors Ltd na Yutong Zhengzhou zimeshauriwa kuanzisha
kiwanda cha magari hapa Nchini kusudimabasi yao yaweze kutengenezwa
na kusambazwa hapahapa nchini.
Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa gari jipya aina ya F12 kutoka kampuni
ya usambazaji ya Benbros Motors Ltd, Waziri wa habari, utamaduni,
Sanaa na michezo Mh. Nape Nnauye amesema Serikali ipo tayari kutoa
ushirikiano wowote ili kufanikisha zoezi hilo.
Amesema, shauku kubwa ya Serikali ni kuona magari aina ya
Yutong sasa yanatengenezwa hapa nchini na kuachana kabisa
na zoezi la kuagiza vifaa kutoka nje ya nchi.
Aidha akizungumzia uzinduzi wa gari jipya aina ya F12
linalotarajiwa kuingizwa sokoni hivi punde, Waziri Nnauye
amekili kuwa gari hilo limekidhi ubora kufuatia kuwa na vitu vyote
muhimu vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Alisema ‘ nimefurahishwa na naomba niwapongeze Benbros Motors
Ltd na Yutong Zhengzhou juu ya uzinduzi wa basi mpya aina
ya F12 Plus, kwani bus hili lina sifa zote kwa barabara zetu na
usalama wa raia.
Amesema sifa za basi hilo jipya, linaitofautisha na mabasi mengine
barabarani na kulifanya liwe mfalme,kwani naambiwa lina uwezo
mkubwa wa kubeba mizigo jambo ambalo linapendwa na abiria
wengi.
Katika hatua Nyingine meneja mauzo
wa Benbros Motors Ltd Bw. Albert Currusa amesema kampuni yake kwa kushirikiana
na kampuni ya Yutong wamejipanga kuendelea kutoa huduma bora kwa Watanzania.
Amesema Basi mpya Aina ya F12 plus inayozinduliwa
ni basi yenye sifa ya kipekee kutoka kampuni ya Yutong ambayo anahakika wateja
wataifurahia ikishaingia sokoni.
Akitaja sifa za basi hilo, Albet
amesema Basi hilo ina uwezo mkubwa wa kubeba mzigo yenye uzito mkubwa, ikiifanya
kuwa mfalme barabarani kwa usafiri ya abiria.
Pia basi hilo linakuja na video za
kisasa ambayo inaitwa (Videoon demand) na ina WifI pia.
Ameongeza Hata kama
Wifi haipatikani bado una uwezo wa kuangalia video, kusiliza radio, kucheza
michezo bure upo Kwahiyo, safari yako itakuwa nzuri tu.
Siti zake zimetengezwa
kwa ngozi kusudi abiria wawe na raha wakati wako ndani ya basi hilo. Screen ya
TV iko kwenye sehemu ambapo abiria anakuwa yuko comfortable. Pia kuna screen
zigine kwa abiria ambao wanakuwa wamekaa nyuma ya basi. Pia kuna port za USB
kusudi abiria aweze kupata burudani ya kutosha.