MBUNGE LEMA AENDELEA KUPATA MATESO,MAHAKAMA YAIRUSHA KESI YAKE TENA,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA,
Godbless Lema leo amefikishwa mahakamani mkoani Arusha na kusomewa shtaka la
uchochezi kwa viongozi wa serikali.
Lema amefikishwa leo mahakamani akiwa tayari amekaa
rumande takribani siku 7 tangu alipokamatwa.
Lema anakabiliwa na shtaka la uchochezi ambapo ni
pamoja na kumtishia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kauli yake
aliyoitoa dhidi ya Rais Dkt Magufuli kuwa Mungu amemuonyesha asipojirekebisha
atafariki.
Baada ya kusomewa shtaka hilo, Lema amerejeshwa
rumande baada ya kukosa dhamana kufuatia pingamizi lililowekwa na upande wa
Jamhuri.
Mahakama imeeleza kuwa itatoa uamuzi kuhusu dhamana
ya Lema Novemba 11 mwaka huu.