MAHAKAMA YAENDELEA KUMTESA MBUNGE LEMA,YAMNYIMA TENA DHAMANA,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo
amefikishwa tena Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa ajili ya kusikiliza rufaa
yake ya maombi ya dhamana.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa mahakamani hapo huku
wafuasi wa Lema wakiwa wamevaa fulana nyeupe zilizoandikwa Jutice 4 Lema
mbele zikiwa na picha yake.
Mbele ya Jaji Fatma Masengi aliyekuwa
amepangwa kusikiliza Rufaa hiyo, Upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiwakilishwa
na mwanasheria Matenus J Marandu umeweka pingamizi kwamba mawakili wa Lema
walipaswa kupeleka notisi ya rufaa kwanza na siyo kukata rufaa
Ulinzi ukiwa umeimarishwa
Wakili wa Chadema Peter Kibatala amesema wao
wameshakamilisha taratibu zote za kisheria, hivyo wanasubiri uamuzi wa
pingamizi hilo lililowekwa na upande wa serikali.
Jaji Fatma Masengi ameutaka upande wa serikali
uwasilishe hoja za pingamizi lao kwa njia ya maandishi kabla ya November
30 ili aweze kutolea uamuzi December 2 mwaka huu.