Zinazobamba

HATIMAYE RAIS MAGUFULI ASAINI SHERIA YA KUNYONGA WANAHABARI,SOMA HAPO KUJUA

 

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, mapema mchana huu wa leo Novemba 17.2016, imetoa taarifa kwa umma juu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa 5 Mjini Dodoma.

Rais Magufuli amesaini Sheria hiyo jana tarehe 16 Novemba, 2016.

Dkt. Magufuli amewapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwa Sheria hiyo.

“Naamini kuwa Sheria hii itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa” amesema Rais Magufuli.

Mwisho wa kunukuu taarifa hiyo kutoka:

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

17 Novemba, 2016