LOWASSA ATOA SABABU YA KUTOKUWEPO KWENYE MSIBA WA SITTA NA MUNGAI,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa
ufafanuzi kuhusu mjadala ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya
kutoonekana kwenye misiba ya aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na waziri
wa Elimu wa zamani, Joseph Mungai.
Sitta alifariki Novemba 7 mwaka huu nchini Ujerumani
alipokuwa ameenda kutibiwa maradhi ya tezi dume ambapo siku iliyofuata
alifariki Mungai.
Lowassa amesema kuwa hakuweza kuhudhuria kwakuwa
alikuwa nchini Afrika Kusini akimuuguza mdogo wake, Bahati Lowassa.
“Mdogo wangu Bahati Lowassa ni ofisa
ubalozi nchini Afrika Kusini, alikuwa anaumwa na alikuwa amelazwa. Kwa siku
zote nilikuwa huko kumuangalia. Nisingeacha kuhudhuria misiba hiyo,”
Lowassa
Mwanasiasa huyo ameongeza kuwa alikuwa pamoja na
waombolezaji kwa kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sitta kupitia
vyombo vya habari pamoja na kumtumia mwanasheria wake kuwasilisha salamu zake
za rambirambi kwa familia ya Mungai.