YAMETIMIA PROFESA LIPUMBA NA MSAJILI WA VYAMA WABURUZWA MAHAKAMANI,SOMAHAPO KUJUA
MGOGORO ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) umeingia
hatua ya pili baada ya Bodi ya Wadhamini kufungua kesi wakimtuhumu Prof.
Ibrahim Lipumba, Jaji Francis Mutungi na watu 12 kwamba, wanahujumu chama
hicho, anaandika Faki Sosi.
Bodi hiyo leo imewasilisha
maombi ya kufungua kesi katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ya
kuomba kibali cha kumzuia Jaji Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini
kutofanya shughuli zake kinyume cha sheria.
Katika kesi hiyo, watuhumiwa ni pamoja na Prof.
Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho aliyerejeshwa kwa barua ya Jaji
Mutungi na watu 12 waliokuwa wanachama wa chama hicho.
Akizungumza na vyombo vya habari Juma Nassoro,
wakili wa chama hicho amesema kuwa, wamewasilisha maombi hayo yaliyopelekwa kwa
Eva Nkya, Msajili wa Mahakama hiyo ambapo ni ombi namba 75.
Wakili Nassoro ameeleza kuwa, katika maombi ya awali
waliyowasilisha kabla ya kesi ya msingi kuanza kusikilizwa ni pamoja na
mahakama kumuamuru Jaji Mutungi kutengua kauli yake ya uteuzi wa Prof.
Lipumba.
Amedai kuwa, mahakama hiyo iliwahi kubainisha kazi
za msajili wa vyama ambapo sio kuingilia uamuzi wa ndani ya vyama vya siasa.
Wakili Nassoro amedai kuwa, Jaji Mtungi hana
mamlaka ya kutengua uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho .
Prof. Lipumba aliandika barua ya kujiuzulu uenyekiti
wa chama hicho Agosti mwaka jana kwa madai ya kutoridhishwa na ujio wa Edward
Lowassa ambaye baadaye aliteuliwa kuwa mgombea urais wa Chadema katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka jana na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa).
Hata hivyo, mwaka huu aliaeleza kuandika barua ya
kutengua barua yake ya wali ya kuziuzulu kwa madai ya kutaka kujenga chama
jambo ambalo limesababisha chama hicho kupasuka.
Wiki iliyopita, Baraza Kuu la Uongozi la CUF, katika
kikao cha dharura kilichofanyika Makao Makuu ya CUF, mjini Zanzibar lilimfukuza
uanachama wa chama hicho Prof. Lipumba.
“Baraza Kuu linaweka bayana kwa wanachama wa CUF,
Watanzania na mamlaka zote nchini kwamba kuanzia leo, Prof. Ibrahim Lipumba
hana haki ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na shughuli zozote za chama,”
ilieleza taarifa ya CUF.
Aidha taarifa hiyo ilidokeza kuwa, uamuzi huo
umechukuliwa baada ya baraza hilo kuridhika na mashtaka dhidi ya Prof. Lipumba
kuongoza na kusimamia kikundi cha wahuni kuvamia Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni,
Dar es Salaam tarehe 24 Septemba, 2016 mwaka huu.
“Baraza kuu limetumia uwezo wake, kwa mujibu wa
Ibara ya 10 (1) (c) na kwa kura zote 43 za wajumbe wake waliohudhuria kumfukuza
uanachama Prof. Ibrahim Lipumba,” ilieleza taarifa hiy