SERIKALI YAANZA KUMCHOKOZA FREEMAN MBOWE,ASEMA KAMA HAKI IKIMINYWA BASI OPARESHENI UKUTA INATARUDI,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Freeman Mbowe amesema Demokrasia, Katiba na Sheria haziheshimiwi na
kwamba Jeshi la Polisi limekuwa wakala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na
kilichofanywa kwenye uchaguzi wa umeya wa Manispaa ya Kinondoni kinawapa sababu
ya kurejea operesheni yao wanayoiita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania
(UKUTA).
Mbowe amesema hayo Oktoba 23, 2016 alipofika eneo
ulipofanyika uchaguzo wa Meya Kinondoni ambapo madiwani wa Ukawa walisusia
uchaguzi huo na kudai kwamba Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Aron Kagurumjuli,
ameshirikiana na CCM kuhujumu zoezi hilo, hivyo wametangaza kwenda mahakamani
kupinga uchaguzi huo baada ya CCM kuendelea na uchaguzi huo na kutangaza
mshindi.
Njama zinazodaiwa kufanywa na mkurugenzi huyo ni
kugawanya madiwani kinyume na kanuni kwa kuhamisha madiwani wa upinzani kwenda
Halmashauri ya Ubungo na kuwahamishia Kinondoni madiwani wa CCM kutoka
halmashauri nyingine.
Mbowe amesema Serikali inaendeshwa kwa hila kwani
licha ya uchaguzi kufanyika siku ambayo si ya kazi, Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo, alikataa barua iliyoandikwa na madiwani Jumamosi Oktoba 22
kuzuia uchaguzi huo kwa kudai kuwa si siku ya kazi.
Aliendelea kwa kumlaumu Rais Dk. John Magufuli
kwamba ameanzisha utamaduni wa kuuwa demokrasia na kwamba analiletea taifa
madhara makubwa.
Kwa upande wake Mbunge wa Kawe, Halima Mdee
(Chadema), amesema wametoka kwenye uchaguzi huo baada ya baadhi ya
madiwani wao kuzuiwa kuingia kwenye kikao hicho.
Mdee alisema kuwa CCM wameingiza madiwani
ambao si wajumbe halali wa kikao hicho kwasabau wanatoka katika halmashauri
zingine.
“Humo ndani yumo Profesa Joyce
Ndalichako ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa na alisajiliwa kama mkazi wa Ilala na
alipiga kura za umeya Ilala hivyo mnaweza kuona uhuni unaofanywa.
“Lakini yumo pia Tulia Akson (Dk. Tulia
Akson, Mbunge wa Kuteuliwa na Naibu Spika) ambaye si mkazi wa Kinondoni yeye
amesajiliwa kama mkazi wa Ubungo,” alisema Mdee.
Amesema kwa mujibu wa kanuni Halmashauri moja
haiwezi kuwa na wabunge wa kuteuliwa zaidi ya watatu na kueleza kuwa katika
kikao hicho wamo wabunge wanne wa kuteuliwa.
Hivyo, kutokana na hali hiyo Mdee amesema watakwenda
mahakama ili kupata tafsiri za kisheria za suala hilo kupata haki.