RC MAKONDA APINGANA NA RAIS MAGUFULI,AIBUKA NA KUAGIZA WAMACHINGA WAONDOLEWE,SOMA HAPO KUJUA
Kufuatia agizo la Rais John Pombe Magufuli miezi
kadhaa iliyopita kutaka kutokubugudhiwa kwa wafanyabiashara ndogondogo maarufu
kama ‘machinga’ na kuachwa waendelee na shughuli zao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda ameeleza kuwa machinga hao wamekuwa wakienda kinyume na
kukiuka tararibu.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Dar es salaam
Makonda ameeleza kuwa machinga wamekuwa wakifanya biashara maeneo yasiyo rasmi
ikiwemo maeneo ya barabara za mwendokasi, nje ya hoteli mbalimbali, vituo vya
daladala na kuwa kikwazo kwa wapita njia, waendesha Bodaboda na baiskeli.
Akiitaja Kariakoo kama mfano Makonda amesema
machinga wamekuwa wakifanya biashara inayofanana na wenye maduka mbele ya
maduka yao jambo linalopelekea wao Kukosa wateja, Huku akieleza kuwa uwepo wa
Machinga umepelekea kutokukusanywa vyema kwa mapato kutokana na kutokuwa na
mfumo maalum ambapo kwa wilaya ya Ilala wamekosa kukusanya bilioni moja ndani
ya mwezi Mmoja, halikadhalika suala la usalama na mali za raia umekuwa Mdogo
kumekuwepo na matukio mengi ya uhalifu.
Hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza machinga wote
kwenda maeneo waliyopangiwa katika wilaya zao na kutoa siku 14 kwa wakuu wa
wilaya kuhakikisha machinga wote wanapelekwa maeneo stahiki.