PROFESA LIPUMBA AENDELEA NA KITUKO CHAKE,SOMA HAPO KUJUA

Kila kukicha mgogoro ndani ya Chama cha Wananchi
(CUF) unazidi kuchukua sura mpya. Jana viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi wamekutana kujadili mgogoro wa CUF sababu ni moja ya vyama
vinavyounda UKAWA.
Viongozi wa UKAWA jana wametangaza kuwa hawamtambui Prof. Lipumba kama mwenyekiti wa CUF na kuwa wao watashirikiana na viongozi halali wa CUF, na kutilia maanani maazimio yaliy0pitishwa katika vikao halali vya CUF.
Viongozi wa UKAWA jana wametangaza kuwa hawamtambui Prof. Lipumba kama mwenyekiti wa CUF na kuwa wao watashirikiana na viongozi halali wa CUF, na kutilia maanani maazimio yaliy0pitishwa katika vikao halali vya CUF.
Aidha, mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe
amewataka viongozi wa chama hicho nchini kote kumpuuza na kutompa ushirikiano
Prof. Lipumba kwani ni msaliti.
Kwa upande wake yeye, Prof. Lipumba ameendelea kutekekelza majukumu yake kama Mwenyekiti wa CUF ambapo jana ametangaza kutengua uteuzi wa Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za Chama cha Wananchi (CUF).
Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa ni pamoja na;-
Joran Bashange – Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha
Ismail Jussa- Mkurugenzi wa Mambo ya Nje
Mustafa Wandwi- Mkurugenzi wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama
Kurufumu Mchuchuli- Mkurugenzi wa Haki za
Binadamu na Sheria
Shaweji Mketo- Naibu Mkurugenzi wa Mipango na
Uchaguzi na
Abdalla Mtolea- Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya
Nje
Aidha Prof. Lipumba amesema kuwa hajali kama
viongozi wa UKAWA wanamtaka au hawamtaki kwani yeye anachojali ni kuijenga CUF.