VITENDO vya Ukatili kwa watoto pamoja na kukithili
kwa vitendo vya Biashara ya Uchagudo vimeongezeka kwa kasi katika mkoa wa
mwanza.Anaandika KAROLI VISENT endelea nayo.
Huku ikonyesha kuwa zaidi ya wasichana 418 katika
mkoa huo wanajihusisha na Biashara ya Uchangudoa
ambapo kati yao wasichana 218
wanaofanya biashara hiyo ni wanawake wenye umri chini ya miaka 18.
Hata hivyo pia imebainishwa kuwa zaidi ya 19,40 ya
watoto ndani ya Mkoa wa Mwanza wanaishi katika mazingira magumu na hatarishi.
Hayo
yemesemwa leo na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Railway Children
Peter Kent wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema katika
utafiti waliofanya katika mkoa wa Mwanza mebaini kuwa watoto ambao
hukumbwa na vitendo vya ukatili katika umri mdogo.
Amesema mara nyingi hali hiyo husababisha mzunguko wa umasikini
zaidi na kuwa katuka hatari zaidi na matokeo hasi ya kimaisha, ambapo utafiti
unaonesha asilimia 100 ya watoto wa mitaani wamewahi kunyanyaswa kimwili au
maneno, huku asilimia ya wasichana na asilimia 25 ya wavulana wamedhalilishwa
kijinsia.
Kent ,amezitaja Takwimu za
utafiti huo kuwa watoto 1940 huishi na kufanya kazi mitaani katika Jiji la
Mwanza likiwa ni ongezeko la asilimia 25 tangu mwaka jana, katika miezi 12 tu
idadi ya wasichana wanaofanya biashara ya ngono kwa asilimia 229.
Huku akidai kuwa hilo ni ongezeko kubwa likiwa ni la wasichana wenye
umri kati ya miaka 11-14, Ambapo idadi ya wasichana wanaofanya biashara ya
ngono ni 418 na kati ya hao 218 ni wenye umri wa chini ya miaka 18, pia
amefafanua kuwa kumekuwepo kwa kupungua kwa asilimia 40 ya watoto wa mitaani
kati ya miaka 0-14 kwa kipindi cha miaka mitatu kwa walengwa.
Sanjari na hayo Mkurugenzi
huyo amezitaja sababu za watoto kuishi katika Mazingira Magumu na kupelekea
kufanya mambo yasiyostahili kuwa ni umasikini, unyanyasaji (UKATILI) na
kutelekezwaongeza, ambapo licha ya juhudi za Serikali wao wameamua kuandaa
Kongamano la Kimataifa walilolipa jina la 'Kuvunja
Mzunguko' litakalofanyika November 17 na 18 katika Ukumbi
wa Benki Kuu ya Tanzania na kutoa fursa ya ushiriki wa wajumbe 250 ambao kwa
pamoja watajadiliana namna ya Kuvunja Mzunguko na kupata uelewa mkubwa wa
Mikakati iliyothibitika ya Kuvunja Mzunguko wa Ukatili kwa familia dhidi ya
watoto wanaoishi mitaani.