MAPYAA YAIBUKA SAKATA LA KAFULILA KUZUILIWA CLOUDS TV,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAKATI aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini,David
kafulila leo akizuiliwa kuongea moja kwa moja kwenye kipindi cha 360
kinachorushwa na kituo cha Luninga cha Clauds Tv kwa kile kilichoelezwa
matatizo ya ufundi ndani ya TV hiyo,
Sasa Mpya yameenza kuibuka juu ya sakata hilo
baada ya kudaiwa kuwa Kiongozi wa juu aliyoko ndani ya utawala wa Rais John
Magufuli ndio amehusika katika kutoa katazo wa kipindi hiko kurushwa hewani.(Fullhabari.blog limedokezwa)
Kafulila ambaye alikuwa mbunge wa NCCR mageuzi leo
alikuwa amealikwa ndani ya Clouds Tv kwa sasa ili kuchambua masuala mbali mbali yanayohusu
hali ya nchi katika kipindi cha 360 kilichotakiwa kuruka hewani majira ya saa
mbili na nusu asubuhi.
Kwa Mujibu wa Mbunge huyo ambaye alisifika kwenye
utawala wa awamu ya nne katika kupambana na kuibua kashfa ya Escrow ambayo iliitikisa
serikali ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kupelekea mawaziri kadhaa kujiuzulu,
Ambapo
amedai alifika kwenye studio na za Kituo hicho zilizopo Mikocheni Jijini dar es
Salaam huku maandalizi mbali mbali ya kipindi hicho kuruka yalikuwa
yamekamilika.
Ameleza maandalizi hayo ni kwa watangazaji wa
kipindi hicho kuanza kutangaza pamoja na wapiga picha kuwa teyari ila gafla ikatokea taarifa kuwa wakubwa wamekizuia kiipindi hicho bila ya kutaja sababu.
Kwa mujibu
wa Mtoa taarifa wa kuaminika kutoka ndani ya Kituo hicho ambaye akutaka jina
litajwe Mtandaoni ameuambia mtandao wa Fulhabari.blogs kuwa shinikizo la kipindi
hicho lilitoka kwa mmoja wa vigogo walioko ndani ya serikali.
“Kaka
sikufichi,kwani leo Kafulila alitakiwa kuzungumza kwenye kipindi chetu ila
tulikuwa tumeshajiandaa kabisa kwa ajili ya kipindi kuruka hewani, kama
unavyojua kipindi kile ni cha moja kwa moja,tukapigiwa simu na watu wa juu serikalini
tukaambiwa tuache kabisa kurusha kipindi hicho,sasa wewe unategemea tufanyaje
kumbuka na sisi tuna watoto wanahitaji kwenye chooni”Kimesema Chanzo hicho.
Ameongeza kusema kuwa kwa sasa wanafanya kazi kwa
uoga mkubwa jambo analodai kama hali ikienda hivyo basi wabunge wa upinzani na
wanaharakati itakuwa vigumu kuitwa kwenye mijadala ya Runinga kwa kuhofia
kufungiwa kwa Vituo vyao,
“Sahivi ndugu tunafanya kazi kwa hofu kubwa sana ,wewe
mwenyewe umeona Redio Five kilichowakuta walimuhoji Mbunge Lema sahivi hawako
hewani,hata kituo cha Itv walimuohi Mbunge Msigwa wakaishia kupigwa Faini ya
mamilioni ye fedha na TCRA,sasa wewe unategemea nini ,sahivi hata sisi tumeanza
kuingiwa na uoga kuwaita wapinzani”ameendelea kuongeza mtoa taarifa huyo.