Zinazobamba

MKEMIA MKUU WA SERIKALI AWAHASA WANAFUNZI NCHINI,SOMA HAPO KUJUA




Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Michael John,akikabidhi cheti na fedha taslimu Sh.450,000 kwa Mwanafunzi wa Sekondari ya Maria De Mattias iliyopo Dodoma,Naomi Sarakikya (kulia) baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kitaifa kidato cha nne somo la Kemia katika shughuli fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkemia mkuu wa serikali nchini (GCLA),Profesa Samwel Manyele



WANAFUNZI nchi wamehaswa kupenda kusoma masomo ya Sayansi ili kuweza kwenda sawa na serikali ya awamu ya tano ambayo imejimbanua kuwa itakuwa serikali ya viwanda.

Ushauri huo umetolewa Mwishoni mwa wiki na Mkemi mkuu wa serikali,Profesa Samweli Manyele wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi wa kidato na cha sita waliofanya vizuri kwenye mtihani wa Kemia.


Amesema ili serikali ya viwanda itimie ipasavyo inatakiwa kwa wanafunzi nchini kijibidiisha katika kusoma masoma ya sayansi ambayo amedai yanaendana na mabadiliko ya viwanda nchini.
“Nawaomba wanafunzi nchi kupenda kusoma masomo ya sayansi ili iweze kuisaidi serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamilia kuwekeza kwenye viwanda,na viwanda haviweze vikaendelea bila ya kuwa na watu wenye ujuzi na masomo ya sanyansi”alisema Profesa Manyele