Zinazobamba

MFUMUKO WA BEI WASHUKA KWA MWEZI WA TISA,OFISI YA TAKWIMU YATOA UFAFANUZI,SOMA HAPO KUJUA





https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_FlMZarX7HuWK-FRr1kRGlxSPyNtDUAR7zHFsWWMfurglY0xrHdVtizrSkvRLrzGViO-HnUh8uix95mP7n0WAAwMb6wPmF7IPBk4w3xSCoxn3kIb05hn5k4sx9Zsa4YQqVpv11ul80OM/s1600/IMG_2959.JPG MFUMUKO wa bei wa umeshuka kwa asilimia 4.5  mwezi Septemba kutoka asilimia 4.9 ya mwezi Agosti mwaka huu kutokana na kupungua kwa upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi uliopita.
Hayo yamebainishwa na  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Ephraim Kwesigabo (Pichani)wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Kwesigabo amesema kuwa kushuka kwa mfumuko wa bei kumetokana na kupungua kwa kasi ya upandajiwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali ikilinganishwa na Mwezi Agosti .


“Mfumuko wa bei mwezi Septemba umeshuka ukilinganisha na mwezi Agosti kutoka asilimia 4.9 hadi kufika asilimia 4.5 kutokana na kushuka kwa upandaji wa bei za bidhaa na huduma”. Alisema Bw. Kwesigabo.
Aidha aliongeza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji Baridi vimepungua hadi kufika asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 mwezi agosti mwaka huu.
Kwesigabo amesema kuwa ushukaji huo wa bei za vyakula na vinywaji baridi umetokana na kupungua kwa kasi ya bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoisha kwa mwezi Septemba mwaka huu.
Mbali na hayo Kwesigabo amesema kuwa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania imefikia shilingi 97.4 katika kununua bidhaa na huduma kwa mezi septemba ikilingfanishwa na shilingi 96.83 mwezi Agosti.

Aidha Mkurugenzi Kwesigabo amesema kuwa anawaomba wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa Ofisi za takwimu Za Mikoa wakati wa ukusanyaji wa takwi,u mbalimbali kwa maendeleo ya nchi yetu.
Habari hii imeandikwa na 
Ally Daud-MAELEZO.