MABALAA YA MIGOMO YAANZA KUNUKIA KATIKA UTAWALA WA RAIS MAGUFULI,WALIMU WAMPA SIKU 15 TU,SOMA HAPO KUJUA
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimetoa siku 15 kwa
Serikali kumaliza madai yao ya muda mrefu vinginevyo watachukua maamuzi magumu.
Rais wa CWT, Gratian Mukoba amesema kuwa uvumilivu
wao umeelekea kufikia ukingoni kwani wamekuwa wakikaa mezani na Serikali mara
kwa mara na kupewa ahadi za kutatua matatizo yao lakini hadi sasa
hazijatekelezwa.
Alisema kuwa Agosti 22 na 23 mwaka huu, Baraza
la chama hicho cha walimu lilipitisha maazimio kupitia kikao chake, maazimio
ambayo yalisainiwa pia na upande wa Serikali kwa ahadi kuwa wangeyafanyia kazi
lakini imeendelea kuwa kimya.
“Siku chache baadae tuliambiwa tusubiri
mchakato wa kuhakiki watumishi ukamilike. Lakini licha ya mchakato huo
kukamilika Serikali imeendelea kukaa Kimya,” Mukoba
anakaririwa na Tanzania Daima.
Aliyataja madai hayo kuwa ni pamoja na posho ya
madaraka kwa wakuu wa shule, muundo wa madaraka, walimu kutopandishwa madaraja
na kulipa madeni ya walimu.
“Ninachoweza kukwambia ni kwamba
mwishoni mwa Oktoba ambao umebakiza siku 15 tutachukua uamuzi mzito ambao
haujawahi kutokea na hatutaki lawakama kutoka sehemu yoyote ile,” alisema
Mukoba.
Rais huyo wa CWT alidai kuwa ingawa Serikali imepiga
hatua katika sera ya elimu bure na madawati, lakini mazingira ya walimu na
ufundishaji yameendelea kuwa magumu hivyo ni vigumu kupandisha ubora wa elimu.