WABUNGE WA CCM WAANZA KUMKATIA TAMAA MAGUFULI,HALI MBAYA YA UCHUMI NA KUONGEZEKA KWA UMASIKINI KWAWACHUKIZA,SOMA HAPO KUJUA
HALI mbaya ya uchumi inaanza kuwaweka pamoja wabunge
wa Tanzania, tayari wameanza kumshughulikia Rais John Magufuli, anaandika
Faki Sosi.
Ilikuwa minong’ono kwa mbunge mmoja
mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulalamikia namna uchumi wa nchi unavyoyumba
miezi michache tangu Rais Magufuli kuingia madarakani, sasa wanaanza kujitokeza
na kuungana na wabunge wa upinzani.
Goodluck Milingwa, Mbunge wa Ulanga Mashariki
amevunja ukimwa ndani ya ukunbi wabunge jana na kuanza kunyooshea kidole
utawala wa Rais Magufuli kwamba, wananchi wanatopea kwenye umasikini.
“Hali ya maisha ni ngumu sana, namuomba Muheshimiwa
Rais hapo aliposhika kwa sababu si mahali pake, hali imekuwa ngumu sana,”
amesema Milingwa akilalamikia umasikini unaokuwa kwa kasi chini ya utawala wa
Rais Magufuli.
Alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia
Muswada wa Sheria ya Taarifa ya Mwaka 2016. Muswada huo uliwasilishwa juzi na
Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria.
Kauli hizo zilikuwa zikitolewa na wabunge ama wadau
wa vyama vya upinzani, taasisi na wasomi mbalimbali nchini.
Milingwa anaungana na mailioni ya Watanzania
wanaolalamikia maisha kuwa magumu zaidi kuliko wakati wa Utawala wa Rais wa
Awamu ya Tano, Dk. Jakaya Kikwete.
Ugumu wa maisha sasa unatambuliwa rasmi na Rais
Magufuli ambapo hivi karibuni alidai kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara
kuchangia hali hiyo kutokana na kutoa fedha zao benki na kukaa nazo majumbani
wao.
Mtikisiko wa uchumi nchini upo dhahiri ambapo juzi
Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo alinukuu taarifa za Benki
Kuu ya Tanzania (BoT) ikionesha namna wananchi wanavyotopea kwenye umasikini
katika uongozi wa Rais Magufuli.
Kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya kiuchumi miezi
michache Rais Magufuli kuingia madarakani, baadhi ya hoteli nchini zimefungwa.
Pia wafanyabiashara wanaotumia Bandari ya Dar es
Salaam wamehamisha mizigo yao na kutumia bandari zingine, madereva wa malori
wakiachwa bila kazi huku kiasi kikubwa cha fedha zinazotokana na kodi zikipotea.
Katika taarifa ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa
Kigoma Mjini aliyoinukuu kutoka BoT na baadaye kusambazwa kwenye mitandao ya
kijamii ameeleza;
a) Taarifa za Benki Kuu zilizopo kwenye tovuti yake
(Quarterly Economic Review na Monthly Economic Review) kwa robo ya mwisho ya
mwaka 2015 (Oktoba – Desemba 2015 ) zinaonesha kuwa kasi ya ukuaji wa Pato la
Taifa ilikuwa 9%. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 (Januari – Machi 2016)
kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilishuka hadi kufikia 5.5%. Kiuchumi, hii
inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi 6 ya
mwanzo ya utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli umepungua kwa 4%.
b) Shughuli za uchumi zinazohusu wananchi masikini
zimeshuka kutoka kasi ya ukuaji ya 10.20% robo ya mwisho ya mwaka 2015 mpaka
2.7% katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ikiwa ni punguzo la 8% ndani ya
kipindi kisichozidi miezi sita. Hii ina maanisha kwamba Wananchi wetu wanazidi
kudumbukia kwenye ufukara kwa kasi tangu awamu ya tano ya Serikali ya Chama
Mapinduzi iingie madarakani
c) Ukuaji wa sekta ya ujenzi katika robo ya mwisho
ya mwaka 2015 ilikuwa 13.8% lakini ukuaji wa sekta hii katika robo ya kwanza ya
mwaka 2016 ilikuwa ni 4.30%, ikiwa ni tofauti ya takribani -10%. Hii ni kwa
sababu uwekezaji katika sekta hii umeanza kushuka.
d) Kasi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji
imeporomoka kutoka kukua kwa 14.50% robo ya mwisho ya 2015 mpaka kukua kwa 7.9%
robo ya kwanza ya 2016, ikiwa ni kuporoka kwa 7% katika kipindi cha miezi 6 tu
ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli. Kuporomoka kwa sekta ya usafirishaji
itaathiri watu wengi, wakiwemo madereva, matingo, pamoja na mama Ntilie
wanaowauzia chakula.