MBUNGE WA CCM ALIYEKAMATWA NA RUSHWA AILILIA SERIKALI MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
KANGI Logala, Mbunge wa Mwibara ameiomba
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa onyo kwa Jamhuri kwa kukwamisha kuwasomea
maelezo ya awali katika kesi inayowakabili, anaandika Faki Sosi.
Lugola, Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Lupa
na Murad Sadiq, Mbunge wa Mvomero wanatuhumiwa kuomba rushwa ya Sh. 30 mil kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Gairo tarehe 15 Machi mwaka huu.
Lugola ametoa
madai hayo leo mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo baada
ya wakili wa serikali Denis Lekayo kueleza kuwa, waendesha mashtaka wa kesi
hiyo hawapo.
Wakili Lekayo
amedai kuwa, shauri hilo liliitishwa kwa ajili maelezo ya awali lakini
waendesha mashtaka hawakupo.
Kutoka na
maelezo hayo Lugola amedai kuwa, ikemee tabia hiyo ya kuahirishwa kesi mara kwa
mara.
Lugola amedai
kuwa, kitendo hicho kinawanyima haki yao ya msingi ya kufanya shughuli zao za
Bunge.
Imekuwa kawaida
kwa washtakiwa wanapokuwa watoro mahakama huwaita kuthibitisha kwa nini wakeshindwa
kuhudhuria.
Baada ya kueleza
hayo, Lekayo ameiomba mahakama radhi na kusema ‘tutafanya haraka kesi
iendelee.’
Hakimu Simba
amesema, kauli iliyotolea na mshitakiwa ni ya msingi. Baada ya kueleza hayo
ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 12 Julai mwaka huu kwa ajili ya kuwasomea
maelezo ya awali
Hakuna maoni
Chapisha Maoni