MAPAMBANO KATI YA UKAWA,CCM,POLISI NA MAGUFULI YAFIKIA PATAMU,UKAWA WAAPA KUFANYA HILI,SOMA HAPO KUJUA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kimepanga kulisaidia Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), anaandika
Pendo Omary.
Hivi karibuni Jeshi la Polisi
lilitoa zuio la mikutano ya siasa ya wazi na ya ndani nchini kote, hata hivyo
CCM imepanga kufanya Mkutano Mkuu tarehe 23 Julai mwaka huu mjini Dodoma.
Kwenye
mkutano huo, Dk. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM atakabidhi mamlaka hayo kwa
Dk. John Magufuli ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa chama hicho.
Baraza
la Vijana wa Chadema (Bavicha) limepanga kuzuia mkutano huo kwa madai ya
kulisaidia Jeshi la Polisi kusimamia agizo lake kwa vyama vya siasa nchini.
Wakizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Slaam viongozi wa Bavicha wamesema,
hatua hiyo ni katika kuhakikisha wanalisaidia jeshi kutekeleza amri iliyotolewa
na Rais Magufuli ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa hadi mwaka 2020.
“Tumeandaa
vijana takribani 2000 kutoka mikoa yote nchini watakaokwenda Dodoma kusaidiana
na Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa CCM. Kwa sababau
Jeshi la Polisi limezuia mikutano yote ya siasa kwa sasa.
“Pia
ni katika kuunga mkono kauli ya Rais Magufuli kwamba, hakuna mikutano ya vyama
vya siasa mpaka mwaka 2020. Huu ndio msiamamo wa baraza.
“Mikutano
yetu sisi kama Chadema tunazuiwa lakini CCM wanafanya. Mahafari ya chama cha
mapinduzi yanafanyika. Ni jana CHASO (Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu
Chadema) Morogoro tumezuiwa lakini UVCCM (Umoja wa Vijana wa CCM) Mkoa wa
Morogogo wamefanya na picha zipo. Hii sio haki, kama mbwai na iwe mbwai,”
amesema Patrick ole Sosopi, Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo.
George
Tito, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya amesema “… ni kwamba, huko mikoani
vijana wameshajipanga. Wana ari kubwa ya kwenda Dodoma.
“Tumeamua
kufikia hatua hii kwa sababu tumekuwa tunaona hakuna haki katika nchi hii. Kuna
mahafali yanafanyika vyuo vikuu, wenzetu CCM wanaruhusiwa sisi Chadema
tunakatazwa.Vijana wa Chadema wamekuwa wakikamatwa bila sababu za msingi,”
amesema Tito.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni