MAKONDA AWAPA RUNGU MADC WAKE,SOMA HAPO KUJUA
PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
amewataka Wakuu wa Wilaya wa Jiji la Dar es Salaam kusimamia Katiba na Sheria
hata kama watachukiwa, anaandika Regina Mkonde
.
“… ningependa wakuu wangu wa
wilaya mchukiwe kwa kufuata sheria, mhakikisheKatiba na Sheria ndiyo kiongozi wenu,” amesema
Makonda leo wakati wa kuwaapisha Wakuu wa Wilaya kwenye Ukumbi wa Karimjee,
jijini Dar es Salaam na kuongeza;
“Kazi
yenu ni kusimama wakurugenzi ili wakamilishe ahadi za rais (Rais John Magufuli)
katika eneo husika. Ni kwamba rais wetu ametupa kazi ya kufanya katikati ya
changamoto nyingi.”
Amewataka
wakuu hao kuhakikisha wilaya zao zinakuwa salama na kwamba, kazi ya ukuu wa
wilaya haina tofauti kubwa ba kazi ya mkuu wa mkoa.
Pia
amewataka kuhakikisha kunakuwepo na vyumba vya madarasa vya kutosha pamoja na
matundu ya vyoo ili wanafunzi waweze kusoma vizuri.
Akizungumzia
usafi wa Jiji la Dar es Salaam amesema “mwezi huu hauwezi kupita bila kuwepo na
sheria ya watupa taka barabarani.
“Wakurugenzi
hakikisheni mnaweka madastibin (vyombo vya taka) ya kutosha, wafanyabiashara
wote kuwa na mahala ya kutupa taka zao,” amesema.
Wilaya
wa Mkoa wa Dar es Salaam walioapishwa wameahidi kukabili changamoto sugu
ikiwemo ardhi, rushwa na ubovu wa miundombinu hususan barabara.
Sophia
Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala amesema kuwa, changamoto ya kwanza
atakayokabiliana nayo ni ile ya ubovu wa barabara na migogoro ya ardhi.
Aidha
Mjema amewataka watumishi wa umma kuzuru katika maeneo yao husika ili kuona
changamoto za wananchi na atakaye shindwa kufanya hivyo, aachie ngazi mapema.
Hashim
Mgandilwa, Mkuu wa Wialaya mpya ya Kigamboni amesema, kwa kuwa wilaya yake ni
mpya atahakikisha anaitangaza ili wananchi wasipate mkanganyiko wanapotaka
msaada.
“Tunajua
wilaya yetu ya kigamboni inaanza, jambo la kwanza nitakaloanza kufanya ni
ugawaji wa kata, hatutaishia hapa mkoa wetu unategemea kigamboni kuwa sehemu ya
utalii,” amesema na kuongeza;
“
Kupitia fursa hii tunatakiwa kipaumble chetu kukiweka katika utalii ili
kuongeza kipato katika halmashauri yetu na pia nitawekeza katika utangazaji wa
wilaya, baada ya hapo ndiyo tutakweda hatua ya pili.”
Kuhusu
gharama kubwa ya nauli ya kivuko cha Daraja la Nyerere, Mgandilwa amesema kuwa,
ataichukua changamoto hiyo na kuipeleka kwenye mamlaka husika ili kujua namna
ya kuipunguza.
Ally
Hapi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amesema kuwa, katika wilaya yake ipo kamati
maalum inayoshughulikia migogoro ya ardhi.
“Ninayo
kamati maalum ya wataalamu wanaohusisha wanansheria, maafisa mipango miji
wanaosikiliza migogoro ya ardhi wilayani kinondoni.Kwakuwa sisi kinondoni ndiyo
nchi, tumeongeza siku ya jumamosi ili kuongeza kasi ya utatuzi wa migogoro ya
ardhi,” amesema.
Felix
Lyaviva, Mkuu wa Wilaya ya Temeke amesema, katika kutokomeza rushwa katika
wilaya yake atatoa namba zake za simu ili kila mwananchi atoe taarifa za
mtumishi anayejihusisha na rushwa.
“Nitatoa
namba yangu mimi ambayo uniambie wakati wowote katika hili niseme kwamba kama
kuna mtumishi wa serikali, taasisi anafikiri rushwa ni sehemu ya maisha yake
atafute pa kwenda,” amesema.
Humphrey
Polepole, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo hakuapishwa kutokana na kutokana na kufiwa
na baba yake mzazi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni