KAULI YA MAGUFULI YAZUA GUMZO,MSIGWA ATAKA IKULU YAKE IUZWE,SOMA HAPO KUJUA
Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa mjini (Chadema)
amemshauri Dk John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuuza
kwanza Ikulu kabla ya kuuza majengo mengine ya serikali ili zipatikane hela za
kuhamia Dodoma, anaandika Josephat Isango.
Msigwa amesema hayo kupitia
ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook na kusisitiza kuwa haamini kama
watanzania ni kama ng’ombe wataswagwa swagwa tu.
“We
have a serious challenge as a National(tunachangamoto hasa kama taifa),
nimshauri Rais aanze kwanza kuuza Ikulu ndipo majengo mengine ya umaa yafuate,
nadhani ikulu itapata wateja mapema , tutapata hela za kuhamia Dodoma.”
Ilisomeka kauli ya Msigwa.
Mbunge
huyo pia amesema haamini kuwa watanzania nikama ng’ombe ambao wataswagwa swagwa
tu wakae kimya, na kuonya kuwa mengi watayaona ambayo bado hayajajiri.
Kauli
ya Msigwa inakuja ikiwa ni wiki tu tangu serikali ya Magufuli kutangaza mpango
wake wa kuhamishia serikali yote mkoani Dodoma kabla ya mwaka 2020.
Magufuli
alitoa kauli hiyo, wakati akihutubia mkutano mkuu maalum wa chama chake – Chama
Cha Mapinduzi (CCM) – tarehe 23 Julai. Mkutano mkuu wa CCM uliomalizika
mkoani Dodoma wiki iliyopita, ulimchagua Dk. Magufuli, kuwa mwenyekiti wa tano
wa chama hicho.
Katika
hotuba yake mbele ya wajumbe, Magufuli ameeleza kile alichoita, “dhamira yake
ya dhati ya kukamilisha mpango wa serikali wa kuhamia Dodoma.”
Uamuzi
wa kuhamishia makao makuu ya serikali mkoani Dodoma, umeonekana kupokelewa kwa
hisia tofauti tangu ulipotangazwa wengi wakisema uamuzi huo unafanyika kwa
papara na bila maandalizi.
Katika
bajeti ya serikali iliyopitishwa na Bunge mwezi uliyopita, hakukutengwa fedha
zozote kwa ajili ya kazi hiyo.