KAMANDA SIRRO AZIGWAYA TUHUMA ZA TUNDU LISSU,NI ILE YA KUWAVUNJA WATU MIGUU,SOMA HAPO KUJUA
JESHI la Polisi kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, limekana kuwa kuna watu waliovunjwa miguu waliopo kwenye chumba cha
watuhumiwa kilichopo kituoni na kusema anayetakiwa kusema kuwa kuna watuhumiwa
waliovunjwa miguu au mikoni ni daktari, anaandika Josephat Isango.
Simon Sirro, Kamanda wa Polisi kanda
maalumu ameliambia MwanaHALISI Online kuwa katika chumba cha watuhumiwa kituoni
humo hana taarifa kama kuna watu waliovunjwa miguu na kama wapo jeshi la polisi
huwa linawapeleka kwenye matibabu.
MwanaHALISI
online lilitaka kupata ufafanuzi ikiwa hao watuhumiwa wanapata haki ya kupata
matibabu na kwanini hawafikishwi mahakamani kwa kipindi kirefu vile kinyume na
sheria za nchi zinavyoelekeza wajibu wa polisi kwa watuhumiwa
.
Sirro
alipoulizwa kuhusu baadhi ya watuhumiwa kukaa muda mrefu bila kufikishwa
mahakamani, alianza kuongea na simu nyingine na kukata ya mwandishi aliyekuwa
na shauku ya kutaka kujua hatima ya hao watuhumiwa.
30 June mwaka
huu akizungumza waandishi wa habari baada ya kuachiwa kwa dhamana, katika
mahakama ya Kisutu, Tundu Lissu Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) aliwataka watetezi wa haki za binadamu na mawakili kupaza
sauti ili haki za hao watanzania ziweze kutambuliwa.
Lissu ambaye pia
ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) aliwataja Abdalah Bushiri, na Adnani
Mohamed Mrutu kutoka Same ambao wamevunjwa miguu na wanateseka katika chumba
hicho bila kufikishwa mahakamani au kupelekwa kwenye matibabu.
“La Pili ni juu
ya wale niliowakuta kule shimoni, na nilioshinda nao usiku wa kuamkia leo, pale
Central kuna watu wamekaa wengine wiki mbili, wengine wiki tatu, na wengine
mwezi, kinyume na sheria ya Tanzania inavyoelekeza kuwa mtuhumiwa afikishwe
mahakamani ndani ya saa 24, isipokuwa kama ni Jumamosi na Jumapili ambazo sio
siku za kazi” alisema Lissu.
“Nilipokuwa
ndani, nimeshuhudia mengi na kweli siku hiyo polisi walikuwa wanahaha, kamanda
wa polisi ametutembelea zaidi ya mara 3 kwa usiku huo” alisisitiza Lissu.
Lissu alilala
mahabusu ya polisi baada ya kuhojiwa na kunyimwa dhamana ambapo siku moja
alifikishwa mahakamani na kusomewa shitaka la uchochezi katika mahakama hiyo.
Kesi yake
inasikilizwa na Hakimu Yohona Yongolo ambapo kwa upande wa mashitaka,
unawakilishwa na Benard Kongolo, wakili wa serikali mkuu huku Lissu akitetewa
na jopo la mawakili zaidi ya kumi wakiongozwa na Michael Ngalo akisaidiwa na
Peter Kibatala.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni