CHADEMA YAMLIPUA MSAJILI WA VYAMA NA OLESENDEKA WA CCM,NI KUHUSU MKAKATI WA UKUTA,SOMA HAPO KUJUA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema
hakina mpango wa kumjibu Jaji Francis Mutungi msajili wa vyama vya siasa nchini
wala Christopher Olesendeka. anaandika Josephat Isango.
Salumu Mwalimu, Naibu Katibu
Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema
Mutungi amejiondolea sifa ya kuwa mlezi wa vyama vya siasa, sababu ameonyesha
upande.
Aidha
kuhusu Christopher Ole Sendeka, Mwalimu amesema hana cheo, hivyo akijitokeza
mwenye cheo Chadema watamjibu.
“Baada
ya Dk John Magufuli, mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kukabidhiwa
alisema sekretarieti yote irudi madarakani, cheo cha msemaji wa chama hakipo
katika katiba ya CCM sisi hatuwezi kujibizana naye” alisema Mwalimu.
Kwa
upande wake, Prof Mwesiga Baregu Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho amesema
licha ya kuwa hawakuwa na mpango wa kujibu Mtungi, ameangalia tamko La Chadema
hakuna popote kama kulikuwa na kauli za uchochezi.
Uchochezi
ni suala kubwa, unapotaja lazima uwe umfanya utafiti na umejiridhisha sio
kutamka tu. Jaji Mutungi huyu ni kijana wangu, tamko lake lina mapungufu mengi.
Alisema.
Katika
hatua nyingine, Chadema imesema itampelekea Mutungi tamko lenye maazimio ya
kamati kuu kuhusu mikutano na operesheni Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania
(Ukuta).
Inaelekea
tamko hilo alilitoa baada ya kusikia au kusoma kwenye vyombo vya habari, kwa
hiyo leo tutampelekea kiofisi kabisa ili aonyeshe yalipo matusi na uchochezi
aliokuwa anasema.
Hata
hivyo chama hicho kimemlaumu Mutungi na kusema ameona tamko la Chadema tu
lakini wakati mikutano inazuiliwa na viongozi wa CCM hakusikika akikemea.
“Kuna
mateso yanaendelea Pemba watu kubambikizwa kesi, mikutano inazuiliwa nchi
nzima, wabunge wetu kule Karatu wamekamatwa kuzuilikuwa kufanya mikutano,
tulitegemea hayo ayasemee, lakini yupo kimya, amejiondolea sifa ya kuwa mlezi
wa vyama vya siasa sababu ameegemea kusaidia CCM”. Alisema Mwalimu.
Wiki
hii mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema moja ya mikakati yao ni
kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.
Alisema
uamuzi huo, ni moja ya maazimio ya Kamati Kuu unalenga kuashiria kupinga kauli
ya Rais John Magufuli na Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa.
Mbali
na mkakati huo, Chadema imeanzisha operesheni iliyopewa jina la Umoja wa
Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta), ikitaja matukio 11 inayodai kuwa ya
ukandamizaji wa demokrasia nchini na mengine 24 yaliyosababisha kuzinduliwa
operesheni Ukuta.
Mutungi
na Ole Sendeka 28 Julai mwaka huu kwa nyakati tofauti
wameibuka wakikituhumu chama Chadema kuwa kimetoa kutoa kauli wanazodai zimejaa
uchochez