![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhiz7aSocKCLpVzUpk1RO0uxD_d_39BJohCZQyo2jksWjAzahxhSJpUfUsnXf-etBh_sZ3uR5dMLh56b60HucX-4VroJ9o5qU1u9OSSx10MbvV7lx4BI8sebTVCg5F1zuDMAe9GabCLSDM/s640/DSC_1988.JPG) |
Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Bw. Afred Mapunda akikabidhi ripoti kwa mwandishi wa habari toka kituo cha EATV mara baada kuzinduliwa. Ripoti hiyo ilijikita katika kuangazia maeneo makuu matu,Ikiwamo suala zima la mikataba kwa waandishi wa habari, Madereva na wabeba mizigo. Katika ripoti hiyo Imebainika kuwa zaidi ya 80% ya waandishi wa habari hawana mikataba ya ajira, wengi wao wanaishi kwa posho. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhKmpGWgy31f7U3G26P_UMufQMuuRTZHaBcPI3IFllMAQlE0G3M2UO9XQAq8lM4S5UV7HGZuhYadsvpr8TnDbQSvN1uDql2yv62-zVwGVAoqmooUu7zHMeMD_uvWYEeFXmvouDwJW2cACo/s640/SAM_0180.JPG) |
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC) Bi. Kijo Bisimba akifafanua kuhusu ripoti ya haki za binadamu na Biashara iliyozinduliwa jana, Bi Bisimba amesema katika ripoti hiyo mengi yameibuliwa ikiwamo baadhi ya Makampuni kuandika Mikataba yake kwa Lugha za Kigeni na hivyo kuwa kikwazo kwa Watanzania kufahamu kilichoandikwa. Mfano Makampuni ya kichina yamediliki Kuandika Mikataba yake kwa Lugha za Kichina. | | |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjKYBY_qHfSvmlJHtdg530WYN4p_b6nxHjMCkFK8KDNhBKY-GcoKwTAgIBpPzPvVN_woo31IWSH2-McJHaTu9RA4AaW4TOp_ybKkFs-T-e4Ol2058pJk7Kc2TNgxFpZwQjvmZSdioWP_wk/s640/DSC_1989.JPG) |
Kaimu Mkurugenzi, Bw Alfred Mapunda akigawa ripoti hiyo kwa wadau waliohudhulia Mkutano huo. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjtbiVFZwInA7l2wOsNi015-pumiTCXSaK_6KkEAMksBp8FRMlPZAaEuH6gm1xQY4DCKcxZbc8yv_SKWtaBYnTFv5t8CYYBJLjIVfPZlr3KFyp30TnqN9myp_MfqAg_3-KbV0vyCIBBCqk/s640/SAM_0206.JPG) |
Kiongozi wa Kundi la watafiti waliohusika katika ripoti hiyo, Mwanasheria Clarence Kipobota akiwasilisha utafiti huo mbele ya wadau mara baada ya kuzinduliwa jana. Adv. Kipobota amesema utafiti huo ulihusisha watafiti 30 ambao walitumia njia za kawaida ili kufanikisha utafiti. Amesema utafiti ulihusisha Mikoa 16 ambayo ni Ruvuma, Morogoro,Geita, Tabora, Arusha,Shinyanga, Kilimanjaro, Daresalaam, Mbeya, Tanga, Mtwara Mara, Mwanza, Dodoma, Lindi na Manyara. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9b90u-Kj7T7brqV02K82OfPTo6SlQzZ33Xiah5dYH8caivb6qkPco7NCwfiNIi3SUmMl0yjDflnwXw2hxMKcfOqcVJWARuUksd3AdV9Jl0VwP1kk8rH3XEi8xQ7bhnQpNZGQUVHZQ39o/s640/SAM_0176.JPG) |
Sehemu ya Watendaji wa Kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC) wakifuatilia uwasilishwaji wa ripoti hiyo kwa wadau. Kwa ujumla ripoti hiyo imeonyesha kuwa jumla ya asilimia 63.8% ya wafanyakazi waliofikiwa katika makampuni yote yaliyofanyiwa tafiti hawana mikataba. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3595WIqNtyu1ML3ANsQNKo3YY9BKuOrWTRurFryfPb5NlZRzHUnott65EgKJeYamJmhWGhGe6HFOx2v_iJXzzu42P4XkS3eNsRvOPh9j4F2GuCBwK_E_TVf0h_Z3yQVbondxpbN7XzL0/s640/DSC_2026.JPG) |
Picha ya pamoja na wadau |
Imebainika kuwa zaidi ya 80% ya waandishi wa habari hawana mikataba, hawana Trade unions hatua iliyotafsiriwa na wadu wengi kuwa ni hatari kufuatia umuhimu wa Tasnia yenyewe ambayo inasadikiwa kuwa muhimili wa nne duniani kote.
Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa ripoti za haki ya Binadamu na biashara, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za Binadamu. Bi. Kijo Bisimba amesema katika utafiti walioufanya walibaini waandishi wengi kukosa mikataba ya kufanya kazi, huku weki wakilipwa kama Vibarua.
Alisema katika utafiti huo licha ya waandishi wa habari kuwa katika hali ngumu ya utendaji wao wa kazi, lakini pia imebainika kuwa wameshindwa kuweza kuwa na umoja wao utakaowasaidia kutatua changamoto zao za kimaslahi ikiwamo mikataba yao.
Ameenda mbele zaidi na kusema mara nyingi waandishi wa habari wamekuwa wepesi kupigania haki za wengine, lakini ni wakati sasa nao waangalie maana wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu ambayo hata akiumwa inakuwa au kuachishwa kazi ghafla ni mzigo kwa familia yake.