ZITTO KABWE AAPA KUPAMBANA NA RAIS MAGUFULI,AMWITA RAIS WA MUHULA MMOJA,SOMA HAPO KUJUA
ZITTO Kabwe, Kiongozi
Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo leo ametoka hadharani na kusema, ‘Rais John
Magufuli ajiandae kuongoza nchi kwa muhula moja,’ anaandika Hamisi Mguta.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Kigoma Mjini amemtabiria Rais Magufuli kuwa, ataweka historia ya kuwa
rais wa muhuma mmoja kwasababu Watanzania hawatamvumilia kuwatawala kwa
kuwaburuza kidikteta.
Zitto
ameibuka leo ikiwa ni siku moja baada ya vyombo vya habari kuripoti kwamba,
kiongozi huyo wa upinzani hajulikani alipo.
Hata
hivyo amesema kuwa, alipata taarifa za kutaka kukamatwa kwake na kwamba,
alichokifanya ni kuonesha kuwa hawezi kukamatwa ‘ovyo ovyo.’
Zitto
ametoa kauli hiyo leo mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za chama hicho
jijini Dar es Salaam.
Kiongozi
huyo amedai kuwa Rais Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonesha udikteta
wake, kitu ambacho hakifai katika demokrasia ya Tanzania.
“Nawahakikishia,
akimalizana na vyama vya siasa atahamia kwenu wanahabari, tumkatalie,”
amewaambia waandishi wa habari waliokuwapo katika mkutano huo.
Hata
hivyo amesema kuwa, hajui kwanini polisi walizuia kongamano la chama chake jana
lililopanga kuchambua Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 katika
Jengo la Millenium Towers, Kijitonyama Dar es Salaam.
”Kama serikali haifanyi sawasawa ni wajibu wetu kuwakosoa, na tutawakosoa kama tulivyokuwa tukifanya kwenye serikali iliyopita…serikali ya sasa haina uvumilivu,” amesema Zitto.
Zitto
amesema, ili kupambana na ufisadi nchini ni lazima Rais Magufuli ampe nguvu ya
kiutendaji Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Seriali nchini (CAG).
Amesema
“CCM wanapaswa kumdhibiti Rais Magufuli na wasipomdhibiti, sisi na Watanzania
tutamdhibiti.”
Amesema,
Jumamosi watu wao wa usalama walimjulisha kuwa Jeshi la Polisi linamsaka ambapo
pia walikwenda nyumbani kwake wakiwa na magari manne ili kumtia nguvuni.
“Jumanne
iliyopita Kamishna Wambura alinipigia simu kuniomba nifike polisi lakini hii ya
Jumaamosi walikuwa wanataka kunivizia, hatufahamu watawala wanaogopa nini mpaka
kuzuia mikutano ya wanasiasa,” amesema Zitto.
Zitto
amesema, suala la kumkamata Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) Mwanza jana kwa sababu ya kawasalimia wananchi, ni
uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia na kwamba, hizo ni
tabia za kidikteta.
”Tunalaani
tabia za kidikteta za Rais Magufuli, ndio maana Magufuli ziara yake ya kwanza
alifanya Rwanda, tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya kudhibiti
Demokrasia na kuongoza kidikteta,” amesema Zitto.
Amesema,
hawatakaa kimya hata kama Rais Magufuli ataamua kuwafunga na kuwa, ‘akimfunga
Zitto, watazaliwa wakina Zitto wengine,’
Amedai
kuwa IGP Ernest Mangu ameagizwa na Rais Magufuli amkamate huku akisema “siwezi
kukamatwa bila kufuata utaratibu.”
”Karibuni
kesho saa tisa kwenye kongamano letu, hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima
tuendelee kufanya siasa, mmeudhuria mikutano yetu hamjaona hata sisimizi
amekanyagwa.
”Sheria
ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 inaruhusu vyama vya siasa kufanya
siasa, makongamano na mikutano ni sehemu ya siasa, hatuhitaji kuomba kibali na
tutaweka utaratibu ili Watanzania wengi zaidi waweze kushiriki kwenye
kongamano,” amesema Zitto.
Amesema,
polisi hawana mamlaka ya kisheria kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na kwamba,
anaipongeza Chadema kufungua kesi ya kikatiba Mwanza huku nao wakidhamiria
kufungua kesi ya namna hiyo jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni