Pichani kushoto ni Katibu mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari mara baada kuzinduliwa Ripoti ya matokeo ya utafiti wa tathmini ya hali ya uongezaji wa virutubisho kwenye Chakula,
Imefahamika kuwa matumizi ya vyakula vyenye
virutubishi na hasa vile muhimu ni fursa pekee ya kuwawezesha wananchi kuwa na afya
bora itakayowawezesha kuzalisha zaidi kwa ustawi wa kaya zao na taifa kwa
ujumla
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya wakati wa uzinduzi wa
ripoti ya matokeo ya utafiti wa tathmini ya hali ya uongezaji wa virutubishi
kwenye vyakula.
Dkt Ulisubisya amesema Takwimu
zinaonyesha kuwa kiwango cha kaya zinazotumia mafuta yaliyoongezwa virutubishi
ni asilimia 54 ambapo unga wa ngano ni asilimia 33.
Amesema lengo kuu la Serikali ni kuboresha zaidi na
kupanua wigo wigo wa matumizi wa vyakula vyenye virutubishi vya vitamin na madini
kwa viwango vinavyokubalika ili kuimarisha afya ya wananchi wote ikiwezekana
kwa asilimia 100.
Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya tano kwa kuelewa umuhimu wa mchango
wa kuongeza virutubishi kwenye vyakula kwa ajili ya kuboresha afya
na lishe ya jamii na kuchangia katika kuinua elimu na uchumi.
Aidha imeondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye virutubishi
vya vitamin na madini vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuja kuongeza
kwenye mafuta ya
kula, unga wa ngano, unga wa ngano, chumvi na vyakula vingine
“Nina imani tutafikia malengo tunayopanga hasa kuhakikisha unga wa mahindi
ambao huliwa na watu wengi hasa wale waishio vijijini unaongezwa virutubishi
muhimu.”Amesema Dkt Ulisubisya.
Alipendekeza matokeo hayo yachukuliwe kama chahchu ya
kitaifa katika kuboresha uongezaji wa virutubishi kwenye vyakula kwa ajili ya uboreshaji
wa afya za wananchi nchini.
Takwimu za awali za kitaifa za afya ya Kidemografia
zilizotolewa hivi karibuni zimeonesha kupungua kwa kiwango cha udumavu kutoka
asilimia 42 mwaka 2010 hadi asilimia 34 mwaka 2015.
Alipendekeza matokeo hayo yachukuliwe kama chahchu ya
kitaifa katika kuboresha uongezaji wa virutubishi kwenye vyakula kwa ajili ya
uboreshaji wa afya za wananchi nchini.
|
Hakuna maoni
Chapisha Maoni