WATANZANIA TUMUUNGE MKONO MWL. NYERERE KWA KUPINGA DHULMA DHIDI YA WAPALESTINA.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Dhehebu la Shia ithnasheriya Sheikh Jalala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya Quds. |
Tukiwa tunaelekea katika maadhimisho ya siku
ya Quds hapo kesho,Kiongozi Mkuu wa Waislamu Dhehebu la Shia ithnasheriya
amewataka watanzania kumuunga mkono baba wa Taifa hili Mwl. Jurius Kambarage
Nyerere kwa kushiriki matembezi ya Quds yanayotarajiwa kuanza hapo kesho.
Sheikh Jalala amesema moja ya sababu kubwa ya
kuunga mkono zoezi hilo ni kutokana na ukweli kuwa toka miaka ya 60, Mwl
Nyerere alikuwa anatambua taifa la Palestina na kuwapa ubalozi hapa nchini.
Amesema, Mwl. Nyerere hakupenda vitendo vya
kibaguzi, dhulma na uonevu wa hali ya juu waliokuwa wakifanyiwa Wapalestina na
kwamba aliamini kuwa wenye Taifa la Palestina ni waarabu Waislamu na wasiokuwa
Waislamu.
Amebainisha baadhi ya madhira wanayofanyiwa
wapalestina ni pamoja na kupokonywa makazi yao,wajawazito kujifungua wakiwa
vizuizini jambo ambalo linapaswa kupingwa vikali na mataifa mbalimbali ikiwamo
Tanzania.
“Ijumaa tutakuwa na zoezi la matembezi kutoka
Ilala boma hadi kigogo, tunawaomba watanzania watuunge mkono kupinga dhulma
wanazofanyiwa wananchi wa Palestina. Hivi sasa hali ni mbaya nyumba Zaidi ya
elfu 48 zimeshabomolewa toka mwaka 1967, kuna wajane ambao hawana makazi,
mayatima na vikongwe wapo katika wakati mgumu sana” Alisema Sheikh Jalala.
Quids ni siku ya Wapalestina na
ukombozi wa mwanadamu Duniani kutoka katika uonevu, ukandamizaji na unyanyasaji
wa mwanadamu. Malengo yake makuu ni kuhamasisha
amani katika nchi hiyo na kuwasaidia wapalestina wapate ukombozi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni