SIMBA CHAWENE AWATAKA WAWEKEZAJI ,WANANCHI KUSHIRIKIANA KUIMARISHA SEKTA YA MADINI
Waziri wa
Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George
Simbachawene (MP) ametoa wito kwa wawekezaji katika sekta ya madini na
wanajamii kufanya kazi kwa ushirikiano ili kukuza amani, utulivu na kuleta
maendeleo ya kijamii.
Waziri aliyasema hayo katika mkutano maalum uliandaliwa na Taasisi ya Uongozi (UONGOZI INSTITUTE) huku akiwakumbusha kufuata taratibu za leseni za kijamii (SLO) kwani kufanya hivyo kutasaidia kuimarisha makazi ya wanavijiji na kuinua mahusiano mema na Makampuni.
Amesema LENGO la leseni ya uchimbaji wa madini(Social licensce operation) ni kuona wananchi wanashiriki katika kupitisha uamuzi wa Kampuni kuchimba madini na hivyo kuongeza uwazi juu ya manufaa ambayo wanaweza kuyapata.
"Migogoro ya kijamii inaweza kusababisha madhara mbalimbali ikiwamo
kuharibika kwa taswira ya Kampuni husika, kupoteza fedha, kutokana na sababu
hizo ndio maana Makampuni yanashauriwa kuwa karibu na wananchi hususani katika
eneo wanalochimba madini ili wakae chini waelewani ni kwa jinsi gani wanaweza
kufaidika na madini yanayochimbwa”. Alisema Simba Chawene
Waziri Chawene amesema sehemu muhimu ya mahusiano ni wananchi kutatuliwa
kero zao ikiwamo fidia zao kutokana na maeneo yao kuchukuliwa, uwezekano wa
kupata ajira na kuweka wazi mipango yote juu ya wananchi wanaouzunguka mgodi
huo kufaidika
Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute,
Mheshimiwa Dennis Rweyemamu, amesema wameamua kuandaa mkutano huo ili kuweza
kubaini changamoto na kurejesha mahusiano mazuri kati ya Jamii na makampuni
yanayowekeza mabilioni ya shilingi
Mtaalamu wa kimataifa kuhusu leseni za Kijamii za uendeshaji Dkt Ian Thomas akizungumza katika mkutano huo. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Uongozi |
Amesema Makampuni katika nchi nyingi, hasa katika nchi
zinazoendelea, huwa wanawekeza mamilioni ya dola katika kuisaidia jamii y,
lakini bado, wanaendelea kukutana na upinzani kutoka jamii jirani hivyo ili
kuondoa tatizo hilo ni vema kukutana na kuweka mazingira mazuri.
Mkutano huo uliwakutanisha zaidi ya wadau 100 kutoka
taasisi mbalimbali za Kiserikali na mashirika ya watu binafsi pamoja na Ngos
Mbalimbali.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni