MEYA WA UKAWA KINONDONI APANIA KULETA MAPINDUZI KINONDONI,ATENGA BILIONI 1.9 KUTATUA CHANGAMOTO YA MADAWATI,SOMA HAPO KUJUA
Boniface Jacob, Meya wa Halmashauri ya Kinondoni |
HALMASHAURIya Manispaa ya Kinondoni imetia saini
mikataba yenye thamani ya Sh. 1.6 bilioni kwa ajili ya kutengeneza madawati
katika Shule za Misingi na Sekondari kwenye manispaa hiyo, anaandika Pendo Omary.
Mikataba hiyo imetiwa saini na
Boniface Jacob, Meya wa Manispaa ya Kinondoni kwa niaba ya manispaa hiyo na
wakandarasi tisa ambapo wanatakiwa kukabidhi madawati hayo mwezi Julai mwaka
huu.
Akizungumza
wakati wa shughuli hiyo, Jacob amesema “mikataba hii yenye thamani ya Sh. 1.6
bilioni itawezesha kutengeneza madawati 12,091 kwa shule za msingi, viti 6,552
na meza 6,552 kwa shule za sekondari. Mpaka kufikia 30 Agosti hakuna mwanafunzi
atakae kaa chini.
“Halmashauri
ya Manispaa ya Kinondoni ameamua kutoa zabuni kwa wakandarasi tisa ili
kuwezesha kazi hiyo kukamilika kwa wakati na kwa ubora utakaolingana na thamani
ya fedha itakayotumika (value for money),” amesema Jacob.
Aidha,
Jacob amesema fedha hizo ni sehemu ya Sh. 1.8 bilioni fedha ambazo zimetokana
na kusimamisha posho za siku tangu mwezi Aprili kwa nafasi za meya, mkurungezi
wa manispaa, wahandisi, ofisa watumishi na wanasheria bila kugusa posho za
madaktrai, manesi na madiwani.
Kampuni
zilizopewa zabuni hiyo ni Msikale itakayotengeneza madawati 500 ya shule za
msingi, meza 500 na viti 500 vya shule za sekondari kwa gharama ya Sh.
87,500,00. Mtweve Worksho itatengeneza madawati 1000 kwa shule za msingi, viti
500 na meza 500 kwa shule za sekondari kwa gharama ya Sh. 132,500,500.
“Pia
Highland Traders and General Services watatengeneza madawati 500 ya shule za
msingi, meza 500 na viti 500 kwa shule za sekondari yenye thamani ya Tsh.
87,500,000. Mai Hardware Supplies atakaetengeneza madawati 500 kwa shule za
msingi na meza 500 kwa shule za sekondari kwa Sh. 87,500,500,” amesema Jacob.
Jacob
ametaja wazabuni wengine kuwa ni Edosama Hardware ambayo itatengeneza madawati
5091 kwa shule za msingi, viti 2052 na meza 2052 kwa shule za sekondari kwa Sh.
662,610,000, Kampuni ya Unipro Solution itatengeneza madawati 2000 kwa shule za
msingi, viti 500 na meza 500 kwa shule za sekondari kwa Sh. 222,500,500.
Wengine
ni Bwanza Investment Company itatengeneza madawati 500 kwa shule za msingi,
viti 500 na meza 500 kwa shule za sekondari kwa Sh. 87,500,500, Benema
Enterprises itatengeneza madawati 500 kwa shule za msingi, viti 500 na meza 500
kwa shule za sekondari kwa Sh. 87,500,500.
“Na
mwingine ni Mazongera Furniture and Decoration Supply, kampuni hii
itakaetengeneza madawati 1500 kwa shule za msingi, viti 100 na meza 1000 kwa
shule za sekondari kwa Sh. 220,000,000,” amesema Jacob.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni