GAVANA WA BENKI KUU NCHINI ATOA NENO,NI KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA YA CHINA KWENYE SOKO LA DUNIA,SOMA HAPO KUJUA
NCHI za Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika
zimepokea kwa furaha hatua ya Benki ya Dunia (WB) kwa hatua ya kuirodhesha pesa ya nchi ya China Yuan kuwa miongoni mwa sarafu
sita duniani ambazo zinaruhusiwiwa kutumika maoene mbali mbali.Anaandika KAROLI
VINSENT endelea nayo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
Salaam,Gavana wa Benki kuu nchini (B.OT)Profesa Beno Ndullu mara baada ya
kumalizika kikao kilichowakutanisha
Magavana kutoka nchi za Afrika na Kusini mwa Afrika ili kujadili hatua
ya fedha ya China kuingia fedha hizo katika soko la dunia.
Ambapo Profesa Ndullu amesema hatua hiyo ni jambo
jema kwani hata nchi inafuika mikopo kutoka China jambo analodai kurodhesha pesa hizo kwenye
soko la Dunia itasaidia kupunguza usumbufu katika kuzibarisha pesa hizo.
Amesema Sarafu hiyo
itazisaidia nchi masikini katika
suala la uchumi kutokana na Makampuni ya China kuiwekeza katika nchi za Afrika
katika viwanda na shuguli nyingi.
Sarafu ya China inaungana na sarafu zengine
kama Dolla,Yemeni,Paund,Swislland,Euro,
ambazo zinatumika katika masoko ya Dunia.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni