WAHAMIHAJI HARAMU 102 WADAKWA DAR,WENGI NI WACHEZA MUZIKI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Kamishna wa Idara ya Uhamiaji mkoani Dar es Salaam, John Msumule picha na Maktaba |
NA KAROLI VINSENT
IDARA ya Uhamiaji mkoani Dar es Salaam imewamata
wahamiaji haramu 102 ambao wameingia nchini pasipo kiharali.
Hata hivyo,pia idara hiyo imewakamata Watanzania
watatu ambao walihusika katika kuwahifadhi wamiaji hao pamoja na kuwazuia
maafisa uhamiaji kutotimiza majukumu yake.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini
hapa,Kamishna wa Idara ya Uhamiaji mkoani Dar es Salaam, John Msumule ambapo
amesema wahamiaji wamekamatwa baada ya idara hiyo kufanya msako mkali ambao
ulianza tangu mwanzoni mwa mwezi na kufanikiwa kuwakamata wahamiajia hao.
Amesema wahamiaji ambao wengi wao wametoka nchi za
India pamoja na Nepal walikamatwa
kwenye Kampuni moja iliyopo Mikocheni wilaya ya Kinondoni Jijini hapa ambapo amedai baada ya kuwakamata na kuwahoji
walibainika wamekuja hapa kwa shughuli za kucheza mziki.
Amesema mara baada ya maofisa wa Uhamiaji kuwataka
waonyeshe kibari cha kuingia nchini ambapo wahamiaji hao walionyesha kubari
ambacho mda wake wa kuishi nchini ulikuwa umekwisha huku wao wakiendelea kuishi
bila ya kutoa taarifa kwenye Idara hiyo.
Hata hivyo,Kamishna Msumule amesema pia Idara yake
inawashikilia watanzania watatu ambao walihusika katika kuwahifadhi wamiaji hao
kwa lengo la kuwaficha watu hao ili mamlaka usika zishindwe kuwakamata pamoja
na kuwatafutia nyaraka zitakazowawezesha kuishi nchini.
Vilevile,amesema Wahamiaji hao pamoja na watanzania
hao,watafikishwa Mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Sanjari na hayo,,Kamishna Msumule amesema Idara yake
inakumbana na changamoto ambazo amedai zinachangia kushindwa kufanya kazi
kikamilifu za kupambana na wahamiaji hao.
Amezitaja Changomoto hizo,Ukosefu wa Magari amabyo
watayatumia kufanya Doria,pamoja uhaba wa Rasirimali watu,hivyo ameiomba
Serikali kutatua changomoto hizo ili Idara hiyo iweze kupambana na wahamiajia
haramu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni