STARA FASHION WEEK YAJA,SOMA HAPO KUJUA
WIKI ya maonysho na Mavazi ya stara, Stara fashion Week 2016 linatazamiwa kuchukua nafasi yake tena mwaka huu katika ukumbi wa City Garden Restaurant Kamata, June 1 hadi 5.
Tamasha
hilo ambalo litafunguliwa na Exhibition ya bure, linakaribisha watu
mbalimbali wanawake wanaume na watoto kwa manunuzi ya vitu mbalimbali,
kama vile Mabaibui,Mitandio Madera kwa ajila ya Mwezi mtufu wa
Ramadhani, evening dresses, kanzu, Udi Hena na vitu vingine pia kutakuwa
na wachora heena kwa bei nafuu.
Exhibition
hiyo ambayo itakuwa inaanza tarehe 1 June asubuhi ya saa nne hadi saa
12 jioni, itafungwa na maonyesho ya mavazi ya stara kwa wanawake pekee
siku ya Jumapili ya tarehe 5 kuanzia saa nne hadi saa 11 jioni.
Katika
kilele cha maonyesho hayo kazi za mikono ya wabunifu wa hapa nyumbani
wanaobuni mavazi ya stara zitaonyeshwa pamoja na warsha itakayojadili
mada mbalimbali ambazo ni pamoja na
1. Jinsi ya kumpata mwenza na kudumisha ndoa
2. Matumizi na Mipango ya Fedha
3. Ujasiriamali Na nyinginezo
Kongamano
hilo la wanawake, litakuwa na kiingilio cha shilling elfu 35 VIP na
Elfu 50 viti maalum Kwa kujumuisha chakula cha mchana kwa wote na zawadi
mbalimbali zitatolewa.
Stara
fashion week imedhaminiwa na TSN group, Maximalipo, Hijab Couture,
Hijabi Central Tz, Kanzu Point, Cordoba School, Speedy Print, I-view
Studio, Vayle Springs, AA Shekhozah co. Ltd, City Garden Restaurant,
Event Lights, Sofia Production, Clouds Media na wengineo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni