SHINDANO LA SHIKA NDINGA LAFIKA TAMATI...WENGI WAPONGEZA, MAKONDA ASIFU EFM RADIO
MKUU WA MKOA WA DARESALAAM, PAUL MAKONDA AKIMUANGALIA ESPEDITO JACKSON BAADA YA KUMKABIDHI FUNGUO TAYARI KWA MATUMIZI YAKE. |
ROSE ANTONY AKIWA KATIKA MCHUANO MKALI WA SHINDANO LA SHIKA NDINGA, MWISHOWE ALIIBUKA MSHINDI NA KUCHUKUA GARI HIYO ALIYOISHIKA. |
MENEJA MKUU WA EFM RADIO (WA KWANZA KUSHOTO)AKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA DARESALAAAM WAKATI ALIPOKUWA ANAZUNGUMZA NA WAAKAZI WA DARESALAAM KATIKA SHINDANO HILO |
SEHEMU YA UMMA ULIOHUDHULIA KATIKA TAMATI YA SHINDANO LA SHIKA NDINGA WAKISHUHUDIA USHINDANI ULIOPO |
MAKONDA AKIWAPONGEZA WALIOZAWADIWA PIKIPIKI |
Hatimaye
SHINDANO la shika ndinga lililokuwa likiendeshwa na kituo cha EFM radio
limefika tamati huku likishuhudia Rose
Antony(23) Mkazi wa Kibaha na Espedito Jackson (Kibaha)wakiibuka washindi wa
shindano hilo na kila mmoja kujinyakulia gari aina ya Suzuki zote zikiwa na
thamani ya shilingi Milioni 20.
Akizungumza
na fullhabari blog Meneja Mkuu wa Efm Radio Bw. Denis Ssebo amesema Kituo chake
kilianzisha shindano hilo kwa dhamira ya kuinua uchumi wa wasikilizaji wake na
kwamba zawadi ambazo wamezitoa zitachangia kuinua uchumi wa washindi hao
Ssebo
Ameongeza kusema mbali na kutoa magari hayo pia wameweza kutoa pikipiki 2 aina
ya Boxer kwa washindi wawili wa kila wilaya ambazo zimeshiriki katika shindano
hilo.
Ametaja
Wilaya ambazo zimeshiriki katika shindano hilo kuwa ni pamoja na Wilaya ya
Kinondoni, Temeke, Ilala, Bagamoyo na Wilaya ya Kibaha ambazo kwa pamoja
wamechukua jumla ya pikipiki 10 zenye Thamani ya Shilingi Milioni 20.
“Leo
tuna furaha tumekamilisha shindano hili na washindi wameonekana, tunaamini
zawadi ambazo tumewapatia leo zitasaidia kuinua uchumi wao… hilo ni jambo zuri
kwetu kwani wasikilizaji wetu hawasikilizi bure wanasikiliza na pia wanafaidika”Aliongeza
Ssebo
MKUU
WA MKOA APONGEZA
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepongeza jitihada zinazofanywa na kituo
cha Efm na kusema shindano hilo litachangia sehemu ya uchumi wanchi.
Alisema
washindi kama watatumia zawadi hizo vizuri kujiingizia Kipato watakuwa
wamejiari wenyewe na Hivyo kuisadia serikali katika suala zima la Ajira.
Amesema
Biashara ya usafiri kwa sasa ni kubwa na inaingiza fedha nyingi hivyo vijana
ambao wamepata gari na wale wenye pikipiki wanaweza kujikwamua kiuchumi na
mwishowe kumiliki Biashara kubwa ya usafiri hapa nchini.
“Leo
mmepewa zawadi hizi za Magali na mapikipiki watu wataanza kuwaganda kwa sababu
mna gari…ninachotaka kuwaambia achaneni na watu wanaowaganda badala yake
jipangeni kutumia vyombo hivi vya moto kuwaletea Kipato” Alisema Makonda
WASHINDI
WATOA YA MOYONI
Katika
hatua nyingine, mmoja wa washindi hao ambaye amejinyakulia zawadi ya juu kabisa
ya gari Ms Rose Antony amesema
amefarijika sana baada ya kufanikiwa kupata zawadi hiyo na kwamba ataitumia
kuhakikisha inamletaea Faida.
Amesema
shindano lilikuwa la wazi na halikuwa lenye upendeleo wowote toka limeanza na
kwamba siri ya ushindi wake ni mazoezi ambayo alikuwa akiyafanya usiku.
“Kuolewa
hapana bado sijaolewa… hiyo haimaniishi kuwa sitafanya biashara… nitahakikisha
biashara hii inakuwa kubwa na inanikwamua kiuchumi ” Alisema
Akizungumzia
ushindani Ms Rose alisema ushindani ulikuwa mkubwa hasa katika fainali kwani
mpinzani wake alimpa wakati mgumu muda wote.
“Wakati
niko kibaha nilisha nafasi ya tatu lakini nikajua wazi kuwa mimi naweza na
nikaamua kufanya mazoezi ya nguvu jambo ambalo limenisaidia kushinda mpambano
huu” Alisema
Hata
hivyo wadau ambao waliwasili katika shindano hilo la shika Ndinga Lililofanyika
viwanja vya TP Sinza, hawakusita kuwapongeza waandaji wa shindano hilo na
kusema limekuwa la uwazi na haki
Wamesema
wameshuhudia mshindi amepatikana hadharani pasipo kuwa na dalili za kuwabeba
baadhi ya watu kitu ambacho kimewatia faraja.
Hamisi
Abdallah ni mmoja wa watu waliohudhuria shindano hilo, amesema ni shindano ambalo
linahitaji kupewa pongezi.
Amesema
namna ya watu walivyoshiriki na hatimaye anapatikana mshindi imekuwa ya wazi na
huru.
Amesema
dhamira ya shindano la shika ndinga ni kuwawezesha kiuchumi wasikilizaji wa EFM
na kwamba sasa ni kazi ya washindi kutumia magari hiyo vizuri ili yaweze
kuwaletea maendeleo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni