RAIS MAGUFULI AENDELEA KUWAPA SHAVU "MAKAPI" WA URAIS CCM,SOMA HAPO KUJUA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu MstaafuMheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda ambaye pia aliwakuwa aliwania nafasi ya Urais ndani ya Chama cha mapinduzi CCM ambapo jina lake lilikatwa katika hatua za awali kabla ya kufika tano bora, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Mei, 2016
Hakuna maoni
Chapisha Maoni