PROFESA LIPUMBA AKATA TAMAA NA UTAWALA WA MAGUFULI,AMTABILIA KUSHINDWA MAPEMA KWENYE UCHUMI,SOMA HAPO KUJUA
Prof. Ibrahim Lipumba (kushoto) alipomtembelea Rais John Magufuli Ikulu mapema baada ya kuapishwa |
PROFESA Ibarahim Lipumba, mchumi mbobezi ndani na
nje ya nchi ameeleza kuchoshwa na utendaji wa Rais John Magufuli katika
kukabiliana na changamoto za kiuchumi, anaandika Regina Mkonde.
Mchumi hiyo aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) kabla ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25
Oktoba mwaka jana ameeleza kwamba, Rais Magufuli ameshindwa kujenga uchumi wa
soko shirikishi.
Prof.
Lipumba ametamka hayo leo mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CUF
iliyopo Buguruni, Dar es Salaam.
Katika
kukabiliana na changamoto za nchi hususani sekta ya uchumi, Prof. Lipumba
amemshauri Rais Magufuli kutafuta ushauri sambamba na taratibu za kujenga
uchumi wa soko shirikishi kutoka kwa Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya
Tatu.
Amesema,
uzoefu wa Rais Mkapa wa kujenga utawala wa serikali unaweza kumsaidia kufanya
uamuzi sahihi utakayosaidia wananchi badala ya kukagandamiza.
Mchumi
huyo ameeleza kuwa, vitisho na ubabe wa Rais Magufuli vinaweza kuwaogopesha
watendaji wake wakiwemo mawaziri na hivyo kushindwa kumueleza hali halisi na
kwamba, kitendo hicho kinaweza kuathiri maendeleo ya nchi.
“Kuna
dalili kwa baadhi ya watendaji wa serikali hasa mawaziri, wakuu wa mikoa na
wilaya za kushindwa kutoa fikra zao zenye lengo la kuimarisha uchumi wa nchi au
kueleza hali halisi iliyopo kwa kuhofia vitisho vya rais ili wasitumbuliwe,”
amesema.
Prof.
Lipumba ametoa kauli hiyo wakati nchi ikiwa kwenye sintofahamu ya upatikanaji
wa sukari ambapo kwa mujibu wake (Lipumba), uhaba huo umesababishwa na agizo la
rais la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.
“Agizo
alilolitoa Rais Magufuli Februari 28, 2016 wakati akiwashukuru waandishi wa
habari, wasanii na makundi yaliyoshiriki kwenye kampeni zake za uchaguzi 2015
ndilo lililosababisha haya,” amesema na kuongeza;
“Kauli
ya serikali ya kuzuia utolewaji wa vibali vya uingizwa wa sukari kutoka nje
ndiyo iliyosababisha upungufu wa sukari, asiuaminishe umma kuwa sababu ni
wafanyabiashara kuficha sukari.
“Kwa
mwenendo huu nchi haitaendelea kutokana na kwamba badala ya vyombo vya dola
kushughulikia masuala ya msingi ili kuleta tija katika maendeleo ya Taifa,
vinahaha kutafuta sukari zilizofichwa.”
Ametoa
mfano wa kitendo cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) cha
kutafuta wafanyabiashara wanaoficha sukari badala ya kushughulika na masuala
nyeti ya ubadhilifu wa mali za umaa kama Tegeta Escrow.
“Wafanyabiashara
wanaopata kibali na wanaopitisha sukari kwa magendo wanapata faida kubwa kwa
sababu bei ya sukari katika soko la dunia mwezi Agosti 2015 ilikuwa Dola za
Marekani 250 kwa tani moja,” amesema.
Amefafanua
kuwa, kama dola moja ni sawa na Sh. 2000 tani moja ya sukari iliuzwa Sh.
500,000 sawa na Sh. 500 kwa kilo moja na kwamba, ukiongeza na gharama za
usafiri kila kilo moja ya sukari itafika kwa Sh. 600.
“Wafanyabiashara
wakubwa na wa kati wanaoingiza sukari nchini hupata faida kubwa ukilinganisha
na viwanda vya ndani kutokana na kwamba, uzalishaji sukari viwandani unagharimu
mtaji mkubwa na kupelekea bei kuwa kubwa na kusababisha kupoteza soko,”
amesema.
Ameshauri
kuwa, kama serikali ina lengo la kulinda viwanda vya ndani ihakikishe inaanda
mfumo wa mnada wa ugawaji wa leseni ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara na
viwanda kupata leseni za kuingiza sukari inayotoka nje ili viwanda vipate
masilahi pamoja na wafanyabiashara.
“Ingawa
utolewaji wa vibali utaathiri viwanda vya ndani kutokana na kushindwa
kushindana na wafanyabiashara, ni vema serikali ikatoa vibali kwa watu wote,”
amesema.
Kama
serikali inataka kujenga uchumi wa viwanda haina budi kutoa motisha kwa
wawekezaji ili wavutiwe kuwekeza katika sekta zote nchini.
“Rais
anahitaji aelewe uchumi wa soko shirikishi, awape nafasi wahusika, asifanye
maamuzi kwenye mikutano ya siasa au hadhara,” amesema.
Habari hiii kwanisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni