MAMBO YAANZA MGEUKA RAIS MAGUFULI,UTUMBUAJI WAKE MAJIPU WAFUNGUA SURA MPYA,SOMA
DHANA ya utumbuaji majipu sasa imemgeukia Rais John
Magufuli kutokana na kuongoza wizara iliyotawala na ubadhirifu wa fedha za
umma, anaandika
Regina Mkonde .
Katika Serikali ya Awamu ya Nne
chini ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Dk. Magufili alikuwa Waziri wa Ujenzi –
wizara ambayo inatajwa kujaa ubadhirifu wa pesa za umma na kwamba, rais huyo ameshindwa
kuchukua hatua.
Kutokana
na hali hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imemtaka Rais Magufuli kutumbua
majipu yake wake wakati akiwa kwenye wizara hiyo.
James
Mbatia, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano amesema, katika wizara hiyo kuna ubadhilifu wa fedha za
umma.
Pia
kumekuwepo na utendaji mbovu wa watumishi na kwamba, serikali haina mpango wa
kuwachukulia hatua za kisheria wahusika kutokana na kutoonesha jitihada.
“Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inajiuliza kama serikali ya awamu ya tano
inafanya kazi yake kwa haki, uadilifu, uwazi na usawa kwa wote na hasa kwa kile
kinachojulikana kama utumbuaji majipu, swali hapa ni nani amfunge paka kengele?
au mkuki mtamu kwa nguruwe mchungu kwa binadamu?” amehoji Mbatia.
Wakati
akitoa hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani leo Bungeni mjini Dodoma kuhusu
mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa
fedha wa 2016/2017 Mbatia amefafanua baadhi ya dosari zilizofanywa na wizara
hiyo.
Moja
kati ya dosari hizo ni kitendo cha Wakala wa Barabara nchini TANROADS cha
kuitia hasara zaidi ya Sh. 5 bilioni serikali.
“TANROADS
imebainika kuwa na utendaji mbovu kama ambavyo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa
hesabu za Serikali (CAG) alivyobaini juu ya usimamizi mbovu katika mikataba ya
ujenzi wa barabaa na madaraja ambapo ilikuwa chini ya iliyokuwa wizara ya
ujenzi katika serikali ya awamu ya nne,” amesema.
Mbatia
ameongeza kuwa “TANROADS wakati wa kipindi hicho, iliitia hasara serikali ya
jumla ya Shilingi
5,616,652,051 kutoka kwenye riba (interest) inayoongezeka
kila siku kutokana na TANROADS kuchelewa kuwalipa wakandarasi 11.”
Amesema
kuwa, hasara hiyo iligundulika kati ya kipindi cha mwaka 2012 na mwaka 2015 kwa
mujibu wa Ripoti ya CAG ya Hesabu za Serikali Kuu wakati wa ukaguzi wa taarifa
za fedha kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2015 iliyotolewa mwezi Machi 2016
(Ukurasa wa 134 na 135).
Dosari
nyingine ni ile ya serikali kuruhusu matumizi ya matairi yanayofahamika kwa
jina la Super single tires ambayo yanaharibu barabara.
“Utafiti
unaonesha matairi haya (super single tyres) yanaharibu barabara. Matairi haya
yameanza kutumika takribani miaka mitano iliyopita na mzigo uliokuwa unabebwa
na matairi 24 sasa unabebwa na matairi 12,” amesema.
Mbatia
amesema, uruhusiwaji wa matumizi ya matairi hayo haukuwa wa busara kutokana na
kwamba matokeo yake ni uharibifu mkubwa wa barabara.
“Uamuzi
wa kuruhusu matairi haya haukuwa na busara maana barabara zetu hazijabuniwa
kuhimili shinikizo la uzito (excessive pressure) linalotokana na matairi hayo,”
amesema.
Ameitaka
serikali kuzuia mara moja matumizi ya matairi hayo ili kuzinusuru barabara
lakini pia kuokoa fedha za walipa kodi zinazotumika kurekebisha mara kwa mara
barabara hizo na kunyima fursa maeneo mengine kupata barabara za kiwango cha
lami.
Akizungumzia
uuzwaji wa nyumba za serikali Mbatia amesema, serikali iliuza nyumba zake kwa
bei ya hasara hivyo kuigharimu nchi.
“Katika
muktadha huo kambi Rasmi ya Upinzani inalikumbusha Bunge kwamba,
kati ya mwaka 2002 mpaka 2004 Serikali iliuza nyumba zipatazo
7,921 na mpaka mwaka 2008 Serikali ilikuwa imejenga nyumba 650 tu,”
amesema.
Amesema
kuwa, katika biashara ya kuuza nyumba zilizokuwa mali ya Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi), serikali ilipata Sh. 252,603,000/-
ambazo
haziendani na thamani halisi ya nyumba hizo.
“Hivi
sasa serikali inahitaji kusaka nyumba zaidi ya mara dufu ya kiasi
hicho kujenga nyumba za fidia.
Kwa
mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya uuzaji wa nyumba
za serikali kinyume cha taratibu, serikali itatumia Sh. 677,606,000/- kujenga
nyumba mpya ili zirejeshwe kwa Tamisemi, Rejea taarifa ya Serikali Bungeni
tarehe 25 April 2008,” amesema.
Mbatia
amesema, waliouziwa nyumba hizo, kuna taarifa kuwa kati yao wapo
walioziuza na kujipatia faida kubwa kinyume na mikataba ya mauzo hayo,na kwamba
KRUB inapendekeza wanyang’anywe nyumba hizo kwa kukiuka mikataba na malengo ya
mauzo.
“Kumbukumbu
za taarifa rasmi za Bunge zinaonesha kwamba, serikali ilitoa taarifa ndani ya
Bunge hili kuwa, kuna kamati iliundwa kuchunguza mchakato wa mauzo ya nyumba ya
serikali.
“Kamati
hiyo ilitegemewa kumaliza kazi mwezi Februari, 2007, lakini hadi Bunge la Tisa
na Bunge la Kumi linamaliza uhai wake hakuna taarifa iliyotolewa na serikali.
Kambi Rasmi ya Upinzani Buneni inaitaka serikali ya awamu ya tano irejeshe
nyumba hizo,” amesema.
Mbatia
amesema, kuna maadhimio kadhaa yaliyoadhimiwa na bunge ikiwemo kuitaka serikali
kurejesha nyumba zilizouzwa kinyume cha taratibu na kwa watu ambao hawakuwa
watumishi wa umma.
“Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni imeiitaka Serikali kutekeleza azimio hilo la Bunge,
na kwa njia hiyo ile kauli mbiu ya hapa kazi tu, iweze kutafsiriwa kwa
vitendo,” amesema na kongeza;
“Tunajua
uuzwaji huo ulisimamiwa na Wizara aliyokuwa akiiongoza yeye na kuna uwezekano
mkubwa kwamba alisimamia maamuzi ambayo hakuwa na uwezo wa kuyakiuka.”
Amesema,
sasa ni muda sahihi Rais Magufuli kurekebisha kasoro alizozisimamia na katika
mchakato huo ili kurejesha imani katika jamii.
“Tukumbuke
kuwa Rais Kikwete alielekeza nyumba hizo zirudishwe serikalini lakini alikosa
uthubutu wa kusimamia kauli yake,” amesema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni