CHADEMA YAMJIA JUU RAIS MAGUFULI,YAMWEKA MTU KATI,NA KUFICHUA MENGI,SOMA HAPO KUJUA
Julius Mwita, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema ( BAVICHA) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Edward Simbeye,Mwenezi BAVICHA na kulia ni Emmanuel Masonga, Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Njombe. |
BARAZA la Vijana wa Chadema
(BAVICHA) limemtaka Rais John Magufuli kuacha kuingilia bunge na kuamuru nini
kijadiliwe, anaandika
Pendo Omary.
Limefikia hatua hiyo ikiwa ni
siku moja baada ya Mussa Azzan Zungu, Mwenyekiti wa Bunge
kuagiza kuondolewa baadhi ya vipengele katika Hotuba ya Godbless
Lema ambaye ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara
ya Mambo ya Ndani.
Vipengele
hivyo vilihusu; mauaji ya viongozi wa kisiasa, mkataba tata wa Lugumi, uuzwaji
wa nyumba za serikali, Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, sakata la vitambulisho vya
taifa (Nida), mwenendo wa rais, kashfa ya ununuzi wa rada na bunge kulinda
walarushwa.
Katika
mkutano na waandishi wa habari leo kwenye Makao Makuu ya chama jijini Dar es
Salaam, Julius Mwita, Katibu Mkuu BAVICHA amesema, “vipengele katika hotuba ya
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni – Wizara ya Mambo ya Ndani
vililazimika kuondolewa bungeni kwa sababu ya Rais John Magufuli.
“Tunashuhudia Rais
Magufuli ndio anaongoza bunge kutoka Ikulu. Baadhi ya wabunge wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wanapigiwa simu na kutishwa akiwemo Livingstone Lusinde, Mbunge
wa Mtera.
“Hata
spika na naibu spika wanapata maelekezo ya kuendesha bunge kutoka kwa rais.
Hotuba hii tutaendelea kuisambaza hadi kila mtu aisome,” amesema Mwita.
Mwita
amesema, kutajwa kwa Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo ya Ndani kudaiwa kuwa
mbia wa Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited, iliyoingia mkataba tata na Jeshi
la Polisi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. 35 Bilioni, ni
sababu tosha ya waziri huyo kuwajibika au Rais Magufuli kutengua uteuzi wake
ili kuipa uhuru Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuchunguza mkataba
huo.
“Tunajua
wazi bunge lingekubali mkataba wa Lugumi ujadiliwe kungemuingiza Kitwanga
kwenye mgogoro. Rais Magufuli ni swahiba wa Kitwanga. Jipu la Lugumi
limeonekana kuwa mwiba. Tunamtaka Rais Magufuli achukue hatua,” amesema Mwita.
Aidha,
Mwita amemtaka Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu kufuta kauli ya kusifia Sheria
ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 aliyoitoa hivi karibuni nchini Uingereza
alipokuwa akizungumza na Watanzania waishio huko kuhusu faida na hasara za
sheria hiyo.
“Kazi
ya jaji yoyote sio kusifu sheria. Anapaswa kutafsiri sheria kwa msingi wa
Katiba. Tunamtaka Jaji Mkuu aondoe tamko hilo haraka. Litasababisha majaji
wengine kushidwa kutafsiri sheria hiyo la sivyo tutaitisha “petition” nchi
nzima kupinga suala hili. Sisi vijana ndio tunaoumia na sheria hii kuliko
makundi mengine,” amesema Mwita.
Katika
mkutano huo Mwita aliongozana na Emmanuel Masonga, Mwenyekiti BAVICHA Mkoa wa
Njombe na Edward Simbeye, Mwenezi BAVICHA
Hakuna maoni
Chapisha Maoni