MAALIM SEIF AMLIPUA DK SHEIN NA CCM YAKE,SOMA HAPO KUJUA
HALI ya
hewa visiwani Zanzibar haijatulia, vidonda vya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe
25 Oktoba mwaka jana vinaendelea kutafuna visiwa hivyo, anaandika Happiness Lidwino.
Maalim Seif Shariff Hamad,
aliyekuwa mgombea urais visiwani humo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) amezidi
kulaani utawala wa Dk. Ali Mohammed Shein kwamba, anaongoza ‘viwiliwili vya
Wazanzibar na si nyoyo zao.’
Maalim
Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF amesema, Dk. Shein anajidanganya kuwa
yeye ni Rais wa Zanzibar na kwamba, wananchi visiwani humo wanamtambua yeye
(Maalim) kuwa rais wao.
“…anajidanganya
tu huyo Dk. Ali Mohammed Shein. Hapa yeye si rais, wananchi walimchagua maalim
na yeye ndiye wanayemtambua kuwa rais wao,” amesema Malim Seif.
Kiongozi
huyo wa CUF ametoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake ya siku nne katika
Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Ametoa
msisitiza kwamba, Zanzibar haina serikali halali na yale yote yanayofanywa visiwani
hapo kwa sasa yanafanywa na utawala haramu wa Dk. Shein.
Hata
hivyo Maalim Seif amesema kwamba, CUF ipo kwenye mkakati wa kufungua mashitaka
kwenye Mahakama ya Kimataifa na kuwa, kinachofanyika kwa sasa ni kukusanya
ushahidi wa kila aina.
Maalim
Seif amewataka viongozi wa chama hicho kuwa tayari kuendelea na msimamo wa
chama hicho na kwamba, ambaye hayupo tayari basi arudishe kadi ya chama hicho.
Kauli
hiyo inatokana na chama hicho kugomea uchaguzi wa marudio uliotangazwa na Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na kufanyika tarehe 20 Machi mwaka huu baada ya
kufuta matokeo halali ya uchaguzi wa mwaka jana unaotajwa kumpa ushindi Maalim
Seif.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni